
ALIYEWAHI kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango nchini Tanzania, Dk. Servacius Likwelile, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumamosi, tarehe 20 Februari 2021, Katika Hospitali ya Regency, jijini Dar es Salaam. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).
Taarifa za kifo hicho, zimetolewa na Vick Kamata, Mke wa Dk. Likwelile, kupitia ukurasa wake wa kijamii, akisema mmewe ameugua kwa muda mfupi.
Vicky ambaye amewahi kuwa mbunge wa viti maalum, ameweka picha ya mmewe na kuandika “nilizani mimi ni jasiri. Lakini kwa hili kumbe mimi si lolote. Mungu mbona umeniachaaaa.”
Dk. Likwelile, alihudumu nafasi za katibu mkuu katika utawala wa Rais mstaafu Jakaya Kikwete hadi alipotenguliwa na tarehe 31 Agosti 2016 na Rais John Magufuli.
Dk. Likwelile alianza kuwa naibu katibu mkuu wa wizara hiyo kabla ya kupandishwa na Kikwete kuwa katibu mkuu.
More Stories
Hizi hapa hoja 10 zinazobeba maridhiano Chadema, CCM
CCM kuanika mazungumzo Rais Samia, Mbowe
Kizaazaa mbunge akiangua kilio, mwingine kupiga sarakasi kisa barabara