Tuesday , 23 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Dk. Kiruswa atoa wiki moja kuweka ‘bicon’ eneo la wawekezaji Kilimanjaro
Habari Mchanganyiko

Dk. Kiruswa atoa wiki moja kuweka ‘bicon’ eneo la wawekezaji Kilimanjaro

Spread the love

NAIBU Waziri wa Madin Dk. Steven Kiruswa ametoa wiki moja kuweka alama (bicon) kwenye mipaka baina ya wawekezaji wawili wa uchimbaji wa madini aina ya Gypsum – Kitivo Investment na Digalla Company ili kuepusha migogoro ya uchimbaji wa madini katika eneo hilo. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Ameyasema hayo wakati akiwa kwenye ziara Mkoani Kilimanjaro katika wilaya ya Same Kata ya Makanya wakati akisuluhisha mgogoro kati ya Mwekezaji wa kampuni ya Kitivo na Mwekezaji Digalla.

Mwekezaji wa Kitivo anamlalamikia mwenzie wa Digalla kumuingilia katika eneo lake la uchimbaji wa madini ya Gypsum na hivyo anataka kampuni ya Digalla kumlipa fidia kutokana na kuchimba Gypsum kwenye eneo lake.

Kwa upande wake mwekezaji wa kampuni ya Digalla amekiri kuingia kwenye eneo la mwenzie bila kujua kutokana na kutokuwepo kwa alama za mipaka ambapo ameahidi kumpa sehemu ya kipande ambayo bado haijachimbwa kutoka kwenye eneo lake kama fidia.

Baada ya suluhisho hilo mwekezaji wa Kitivo Investment amekubali fidia hiyo kutoka Kampuni ya Digalla.

Aidha, Mkuu wa wilaya ya Same, Kasilda Mgeni amewataka wawekazaji hao kushirikiana kwa pamoja katika kujenga uchumi wa Taifa letu na wachimbaji wengine wote kuzifanyia ukarabati barabara ambazo Maroli yao yanapita hili Wananchi wasipate tabu kupita kufata huduma za kijamii 

Mbalimbali na hayo yote Afisa Madini Mkoa kilimanjaro Fatma kyondo amewasisitizia wachimbaji hao kuzingatia kanuni na sheria za uchimbaji wa Madini.

“Nakuakikisha wanafukia mashimo kwa haraka maeneo ambayo yamechimbwa Mawe hayo ili kuepusha madhara yanayoweza kutokea, na yeyote asiyewajibika kufanya hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake”alisema Kyondo

Pamoja na hayo Naibu Waziri wa Madini,Kiruswa amemugiza Afisa wa Madini Mkoa Kilimanjaro Fatma Kyondo kuwasimamia wawekezani hao wakati wakikabidhiana fidia iliyoahidiwa ili kumaliza mgogoro huo.

Wawekazaji hao wameshukuru ujio wa Naibu Waziri na kuweza kutatua Mgogoro huo na wameahidi kutotokea tena mgogoro baina yao.

Aidha, wameahidi kuweka alama za mipaka (bicon) kama walivyoelekezwa ili kuendelea kukuza Uchumi wa nchi ambapo pia wamemshukuru Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuamini wachimbaji wadogo wa Madini ya Gypsum.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

Habari Mchanganyiko

DC ampongeza Dk. Rose Rwakatare kwa kusaidia waathirika wa mafuriko Mlimba

Spread the loveMWENYEKITI wa Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk.  Rose Rwakatare...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the loveMBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi...

error: Content is protected !!