Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Dk. Kimei akataa kung’ang’ania madaraka
Habari Mchanganyiko

Dk. Kimei akataa kung’ang’ania madaraka

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk Charles Kimei
Spread the love

MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei amesema hatoongeza muda wa kuiongoza taasisi hiyo baada ya mkataba wake kukamilika Mei, 2019, anaandika Mwandishi Wetu.

Kimei atakayekuwa ameiongoza CRDB kwa miaka 21 atakapostaafu, amesema uamuzi huo anaufanya kupisha damu mpya kuendeleza mafanikio ya benki hiyo kubwa nchini.

“Si vizuri kung’ang’ania madaraka. Tunao wakurugenzi tuliowaandaa kwa muda mrefu ambao wanaweza kuendeleza nitakapoishia. Ninapisha damu changa nami nitaendelea kuwa mwanahisa wa kawaida,” amesema Dk Kimei leo Alhamisi Desemba 28,2017.

Kwa utaratibu wa benki hiyo, mchakato wa kumpata mkurugenzi mtendaji huchukua miezi 18 lakini Dk. Kimei ameongeza mwezi mmoja na kuifanya 19 ili kuipa bodi ya wakurugenzi nafasi zaidi ya kukamilisha hatua hizo.

Amesema ingawa upo mfumo mzuri wa kurithishana madaraka ndani ya benki hiyo, lakini mwenyekiti na bodi wana uhuru wa kumchagua mtu mwenye sifa za ziada kutoka nje na kushirikiana na familia ya benki kuendeleza mafanikio.

“Katiba yetu inataka Mtanzania ndiye aiongoze CRDB. Ninaiamini timu niliyoshirikiana nayo tangu niingie hapa. Hata benki nyingine zinazotafuta wakurugenzi watendaji, ningezishauri zije CRDB,” amesema.

Ndani ya muda uliobaki kabla mkurugenzi mpya hajakaribishwa, Dk Kimei amesema angependa kuona inapata faida kama ya mwaka 2015 ilipotengeneza Sh 187 bilioni ikiongezeka kutoka Sh 148 bilioni mwaka 2014.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awataka wahariri kufanya kazi bila uoga, upendeleo

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amewataka wahariri wa vyombo...

Habari Mchanganyiko

STAMICO yasaini mkataba wa bilioni 55.2 kuchoronga miamba GGML

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limezidi kufanya vizuri katika...

Habari Mchanganyiko

NMB yatoa traksuti za Mwenge wa Uhuru Mtwara

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa traksuti kwa mkoa wa Mtwara ambako...

Habari Mchanganyiko

Yara yaja na bima ya mazao kwa wakulima

Spread the love  WAKATI serikali ikiweka mikakati mbalimbali kuimarisha sekta ya kilimo...

error: Content is protected !!