Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Kikwete: Msikubali kutumika
Habari za SiasaTangulizi

Dk. Kikwete: Msikubali kutumika

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete
Spread the love

 

RAIS Mstaafu wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete, amewashauri Watanzania wasikubali kutumika katika kutengeneza migogoro. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Rais huyo wa Awamu ya Nne wa Tanzania, ametoa wito huo leo Ijumaa tarehe 21 Mei 2021, katika Kongamano la Maadhimisho ya maiaka 40 ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), liliofanyika mkoani Dar es Saalam.

Mwanasiasa huyo ametoa ushauri huo akizungumzia migogoro ya rasilimali, inayotokea barabani Afrika.

Akizungumzia migogoro hiyo, Dk. Kikwete amesema kuna baadhi ya migogoro huchochewa na watu ambao huwa mstari wa mbele kujifanya wasuluhishi wake, na kuwashauri Watanzania kuwa makini na watu wa namna hiyo.

“Wakati mmoja nilishughulikia mgogoro mmoja, siitaji nchi hiyo. Mtu mmoja akaniambia huko mnakokwenda kusuluhisha mgogoro hawa mnaofuatana nao wako upande ule wanauchochechea,”amesema Dk. Kikwete.

Mwanasiasa huyo amesema “kwa hiyo kuna mazingira hayo, lakini muhimu sisi wenyewe kubaini kiasi gani tusikubali kutumika kwa ajili ya masilahi ya wtauw engine ili tutumike wka ajili ya msilahi yetu sisi wenyewe.”

Dk. Kikwete amesema migogoro mingi ya rasilimali za nchi husababishwa na watu wenye tamaa, kutoka ndani au nje ya nchi husika.

“Migogoro ya rasilimali ina mchanganyiko wa mambo mengi, wakati mwingine tamaa zetu wenyewe kwamba pale ikipatikana mafuta na gesi unasahau ni rasilimali ya Taifa. Unakaa pale unasema gesi haitoki, mkisha kuwa kila mtu alichokuwa nacho ni kwa ajili yake yeye tu, kutakuwa hamna Taifa,” amesema Rais Kikwete.

Dk. Kikwete amesema “sura nyingine husababishwa na wanaotamani hizo rasilimali, wanatengeneza mgogoro halafu wao wanakuja kutenegeneza usuluhishi, na mgogoro wanauchochea wao.”

Katika mada hiyo, Dk. Kikwete alikumbushia mgogoro wa gesi ulioibuka 2013, kati ya Serikali na wananchi wa mikoa ya Kusini, hasa Mtwara.

“Ndiyo maana tulipata tabu sana pale mwanzoni shemeji zangu Wamakonde walivyosema gesi haitoki Mtwara, wakati mwingine ningenufaika sababu mke wangu (Salma Kikwete) ni mtu wa huko. Lakini tulikataa,” amesema Dk. Kikwete.

Akisumulia mkasa huo, Dk. Kikwete amesema mgogoro huo ulisababishwa na baadhi ya wanasiasa wa mikoa ile, huku akisema alifanikiwa kuudhibiti kwa kuwashikisha adabu walioshiriki.

“ Wakati mwingine yanachochewa na wanasiasa wa pale pale, na ndiyo maana nilipokuwa rais baadhi yao ilibibidi kuwashikisha adabu tu. Walikuwa wabunge nikasema washikisheni adabu siku moja, ili tuweke akili kwamba hizi ni rasilimali ni za Taifa,” amesema Dk. Kikwete.

1 Comment

  • Safari zake za nje ziligharimu kiasi gani? Ni faida kiasi gani ilipatikana? Si ajabu aliitwa Vasco da Gama. Kila mwezi kumtembelea rafki yake Obama akifuatana na msururo. Mpaka barabara ya Ikulu ikapewa jina na Obama

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!