Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Kijaji awatahadharisha Maofisa Ugavi
Habari za Siasa

Dk. Kijaji awatahadharisha Maofisa Ugavi

Naibu Waziri wa Fedha, Dk. Ashantu Kijaji
Spread the love

SERIKALI imetangaza kuwa kuwachukulia hatua kali Maofisa Ununuzi na Ugavi ambao wamekuwa wakishindwa kufuata Sheria za manunuzi na kuisababishia serikali kupata hasara. Anaripoti Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Hayo yalielezwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashantu Kijaji wakati wa ufunguzi wa kongamano la Mwaka la Bodi ya wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB).

Akizungumza na wataalamu hao alisema kuwa serikali hatuwezi kufikia uchumi wa kati na uchumi wa viwanda kama ilivyo sera ya serikali kama wataalamu hao wanaweza kukiuka Sheria ya manunuzi kwa kufanya udanganyifu katika kazi zao.

Naibu huyo alisema kuwa alisema kuwa njia pekee na nguzo ambayo inaweza kusababisha kuwepo kwa maendeleo ni wataalamu hao kuwa wabunifu na kuzingatia kanuni na sheria ambazo zinaendana na manunuzi.

Mbali na hilo alisema kuwa wapo wataalamu wa manunuzi ambao wamekuwa wakisababisha kuwepo kwa malalamiko na kusababisha wananchi kuichukia serikali kutokana na tabia ya wataalamu hao kutokuwa waaminifu katika kazi zao.

“Ili kufikia malengo ya maendeleo ya uchumi wa viwanda na uchumi wa kati ni lazima wataalamu wa Ununuzi na Ugavi  inapasuka wataalamu hao wakatanguliza uzalendo katika kazi zao bila kutanguliza maslahi yao binafsi.

“Lakini napenda kusema kuwa imekuwa ni aibu kwa halmashauri mbalimbali kuwa na ripoti mabaya ya Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) kutokana na miradi mingi inayofanyika kutokuwa na kiwango kinacholingana na thamani ya fedha na kwa hali hiyo basi kwa sasa tunayo taarifa ya baadhi ya watu ambao wamekuwa wakikiuka Sheria ya manunuzi na kujiwekea Sheria ya kwao na sijui Sheria hiyo wameitoa wapi?” alihoji Dk. Kijaji.

Naye Mwenyekiti wa bodi ya wataalamu wa ununuzi na Ugavi, Dk.Heren Bandiho, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasm katika uzinduzi huo, alisema malengo ya bodi hiyo ni kuhakikisha inainua uchumi wa kati na uchumi wa viwanda ifikapo Mwaka 2025.

Alisema kuwa uweledi wa wataalamu wa Ununuzi na Ugavi nchini ndiyo roho upatikanaji wa maendeleo ikiwa ni pamoja na kufanya manunuzi ambayo yanaendana na Sheria ya manunuzi sambamba na kufanya miradi bora ambayo inaendana na thamani ya fedha.

Pamoja na mambo mengine Dk.Bandiho alisema kuna changamoto ya baadhi ya Wakili kuwaajiri wataalamu wa ununuzi na Ugavi ambao Havana viwanga na hawajasaliliwa na bodi.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia atua Uturuki kwa ziara ya siku 5

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumatano amewasili nchini Uturuki kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Samia arejesha mikopo ya 10%, bilioni 227.96 zatengwa

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amerejesha utaratibu wa utoaji mikopo...

Habari za Siasa

Rais Samia amfariji mjane wa Musa Abdulrahman

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumanne amempa pole Mwanakheri Mussa...

error: Content is protected !!