Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Kigwangalla atiwa matatani tena
Habari za SiasaTangulizi

Dk. Kigwangalla atiwa matatani tena

Spread the love

 

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk. Damas Ndumbaro, ametengua uamuzi wa mtangulizi wake, Dk. Hamis Kigwangalla, wa kufuta umiliki wa kitalu cha Uwindaji cha Lake Natron Game Controlled Area East, kutoka kwa Kampuni ya Uwindaji ya Green Mile Safaris Limited. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Dk. Ndumbaro ametangaza uamuzi huo leo Alhamisi tarehe 29 Aprili 2021, akitoa taarifa ya mapitio kuhusu uamuzi wa Dk. Kigwangalla, aliyekuwa waziri wa maliasili na utalii wakati wa kufutwa kwa umiliki wa kitalu hicho.

Dk. Ndumbaro amesema, ametengua uamuzi huo kwa kuwa, uamuzi wa Dk. Kiwangalla haukuzingatia sheria na misingi ya utawala bora.

“Kufuatia uchambuzi uliofanyika kuhusu uamuzi wa kufutiwa umiliki wa kitalu cha Lake Natron – East, nimejiridhisha, malalamiko ya muomba mapitio yana msingi wa kisheria.”

“Barua ya Mhe. Waziri (Dk. Kigwangalla) ya kufuta umiliki wa kitalu, haikuzingatia sheria na misingi ya utawala bora,” amesema, Dk. Ndumbaro.

           Soma zaidi:-

Kutokana na hatua hiyo, Dk. Ndumbaro amesema, “ninaamua na kuagiza muomba mapitio (Green Miles Safaris Limited) arejeshewe umiliki wa kitalu cha Lake Natron Game Contolled Area-East hadi mwaka 2022.”

Dk. Ndumbaro ambaye kitaaluma ni mwanasheria amesema, Dk. Kigwangalla alichukua uamuzi huo pasina kumueleza kosa mhusika, wala kumpa nafasi ya kujieleza, kinyume na sheria.

“Mbele yangu, sina ushahidi unaonesha kuwa kabla ya kufutiwa umilikiwa kitalu cha uwindaji, muomba mapitio alijulishwa kosa lake na kupewa sababu za uamuzi kama ambavyo kifungu cha sheria kinataka.”

“Barua ya waziri, inaelezea mamlaka yake katika kufuta umiliki wa kitalu lakini hailezei kosa ambalo muomba mapitio amelitenda,” amesema Dk. Ndumbaro, ambaye ni Mbunge wa Songea Mjini (CCM).

Amesema, uamuzi huo umechukuliwa baada ya kampuni hiyo kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa Dk. Kigwangalla alioutoa kwa barua yake ya tarehe 7 Agosti 2019.

Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Tanzania, Dk. Hamisi Kigwangalla

Uamuzi huo wa Dk. Ndumbaro, ameutoa kipindi ambacho mtangulizi wake huyo, Dk. Kigwangalla akiwa amewekwa matatani na ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka wa fedha wa 2019/2020.

Ripoti hiyo ya CAG, Charles Kichere iliwasilishwa bungeni tarehe 8 Aprili 2020, ilionyesha kuwa, tamasha la Urithi Festival lililofanyika mwaka 2019, kulikuwa na viashiria vya ubadhirifu wa fedha kutokana na kanuni mbalimbali kukiukwa.

Tamasha hilo lilifanyika chini ya uongozi wa Dk. Kigwangalla wakati akiwa waziri wa maliasili na utalii.

CAG Kichere alisema, fedha zilizotumika kufanikisha tamasha hilo, hazikuwa katika bajeti ya wizara hiyo, wala hakukuwa na mpango ulioidhinishwa wa utekelezaji wake.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Damas Ndumbaro

Alisema, kutokana na fedha hizo kuwa nje ya bajeti, wizara hiyo ilichangisha kiasi cha Sh.1 bilioni kutoka katika wakala zake nne ambazo ni Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Wakala wa Huduma za Misitu (TFS), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na Mamlaka ya Usimamizi wanyapori Tanzania (TAWA).

“Kulikuwa hakuna mpango wa utekelezaji wa tamasha la utalii. Kutokana na kukosekana kwa mpango wa utekelezaji uliodhinishwa, nilibaini kuwa wizara ya malialsili na utalii iliomba wakala zake nne kuchangia.”

“Kila moja ilitakiwa kuchangia Sh. 250 Mil ambazo hazikuwa kwenye bajeti zao, ili kuwezesha kufanyika kwa tamasha hilo,” alisema CAG Kichere.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!