July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Kebwe: Wataalum wa mionzi wapo 517

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Kebwe Stephen Kebwe

Spread the love

NAIBU Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Kebwe Stephen Kebwe, amesema Tanzania ina wataalamu 517 wa mionzi, ambapo kati yao 59 ni madaktari bingwa. Anaandika Dany Tibason …(endelea).

Amesema kuwa, bado kuna changamoto katika sekta hiyo na serikali inalifanyia kazi jambo hilo.

Dk. Kebwe alitoa kauli hiyo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Anastazia Wambura (CCM), ambaye alitaka kujua kama serikali ina taarifa kuwa kuna upungufu wa wataalamu wa mionzi.

Mbunge huyo alihoji kama inayo taarifa ni wataalamu wangapi walipo hivi sasa kwa nchi nzima na akahoji masomo ya kozi hiyo ni kwa muda gani.

Naibu waziri amesema kuna changamoto kubwa katika kada ya mionzi na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeendelea kuifanyia kazi ikiwemo kuendesha mafunzo ya astashahada, stashahada na stashahada ya juu ingawa wahitimu watarajiwa wamekuwa ni wachache.

Amesema katika kipindi cha mwak 2014/15, jumla ya madaktari bingwa wa mionzi (radiogists) walikuwa 59 kwa nchi nzima, madaktari wasaidizi 47, maafisa wenye shahada ya radiografa 40, wateknolojia 408 wakati wateknolojia radiografa waliokuwa katika ngazi ya astashahada walikuwa 22.

Kwa mujibu wa Dk. Kebwe, sambamba na kuboresha mafunzo na pia kuendana na mpango wa afya ya msingi, wizara imepitia mitaala mbalimbali ya mafunzo kulingana na mabadiriko katika sekta ya afya kwa nia ya kuboresha mafunzo.

error: Content is protected !!