January 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Kawambwa abanwa bungeni kuhusu vyuo

Chuo Kikuu cha Dodoma

Spread the love

MBUNGE wa Jimbo la Dodoma Mjini Dk David Malole,(CCM)  ameitaka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kutoa majibu ya kina ni namna gani inavyowatumia wasomi wa vyuo vikuu Dodoma (UDOM) St.John’s  kuboresha kiwango cha elimu. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Dk. Malole alitoa kauli hiyo katika swali lake ambapo amesema  mpango wa kuwapanga wanavyuo hao ambao wengi wanasoma vitivo vya elimu akataka wapangwe katika shule mbalimbali za Dodoma kama sehemu ya kuwatia moyo wananchi wanaozunguka vyuo hivyo.

Akijibu swali hilo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa amesema  wanafunzi hao hupangwa kufundisha kwa vitendo katika shule mbalimbali kwa ajili ya kufanya mazoezi.

“Hata hivyo, mahali pa kufanyia mazoezi ya kufundishia ni suala la utashi wa wanafunzi kabla ya kupangiwa, wanafunzi hutakiwa kuchagua mikoa mitatu na shule tatu ambazo wangependa kufanya mazoezi ya kufundishia,” amesema  Kawambwa.

Dk.Kawambwa amesema  muongozo  wa mazoezi ya kufundisha kwa vyuo vya St John’s na Udom, vimekuwa vikipangiwa walimu-wanafunzi kufanya mazoezi ya kufundisha katika shule za halmashauri zilizopo mkoani.

“Kwa mfano, mwaka 2012, Chuo Kikuu cha St John’s kilipangiwa wanafunzi 325 (200 sanaa,125) sayansi) na mwaka 2013 walipangiwa wanafunzi 249 (176 sanaa, 77 sayansi),” amesema

Kwa upande wa Udom amesema  mwaka 2013 kilipangia walimu wanafunzi 114 katika shule mbalimbali kwa mkoa wa Dodoma kufanya mazoezi ya kufundishia.

Kwa mujibu wa Waziri mazoezi ya kufundishia huwa yanafanywa kwa kuzingatia muongozo wa mazoezi ya kufundishia  ambamo kila chuo huwapangia wanafunzi wanaosoma program za ualimu katika shule mbalimbali kwa ajili ya kufanya.

error: Content is protected !!