January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Kashililah amuumbua mbunge wa Singida

Spread the love

KATIBU wa Bunge Dk.Thomas Kashilillah amesema kuwa, hadi sasa hajapokea barua ya mbunge yeyote ya kukataa kupokea posho za vikao vya Bunge (Sitting alowances). Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Dk. Kashilillah alitoa kauli hiyo wakati alipozungumza na mwanahalisionline mjini hapa, kuhusu taarifa za baadhi ya wabunge kudai kukataa fedha hizo na baadala yake zielekezwe kwenye shughuli za maendeleo ya jamii.

Ni siku motu imepita baada ya Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu alidai kuiandikia barua ofisi ya bunge kueleza kuwa, hatochukua posho hizo na badala yake zielekezwe katika maendeleo ya jimbo.

Dk. Kashilila amesema, ofisi yake iko wazi, tayari kupokea barua ya mbunge yoyote ambaye anakusudia kuandika barua ya aina hiyo kwa ajili ya kufanyiwa kazi kulingana na maudhui hayo.

“Sisi tupo ofisini na hatujapokea barua yoyote, hatuwezi kufanya kazi kwa kutumia magazeti au mitandao ya kijamii kwani kwa kufanya hivyo tutakuwa tunakosea.

“Kama kuna mtu anataka asipokee hiyo posho, tutaona jinsi ya kufanya lakini hatuwezi kumzuia mtu asifanye vile anavyotaka, ni matakwa ya mtu mmoja mmoja,” amesema Dk. Kashilila.

Amesema iwapo mbunge ataandika basi itakuwa utashi wake mwenyewe na si wa wengine “kwani wewe ofisini kwako ukisema hutaki kupokea mshahara, watakulazimisha?, kwani wewe ukikataa mshahara na wengine watakataa” alihoji.

Mbunge mwingine ambayewahi kutangaza kutopokea posho hizo ni Zitto Kabwe wakatia akiwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia Chadema.

error: Content is protected !!