April 14, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Kalemani awaka Watanzania kuchangamkia ajira Bombala Mafuta

Dk. Medard Kalemani, Waziri wa Nishati

Spread the love

WAZIRI wa Nishati Dk. Medard Kalemani amewataka wananchi na wadau wa mkoa  wa Kagera kuwa na utayari katika kuchangamkia fursa na ajira wakati mradi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) utakapokuwa unatekelezwa kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga wenye urefu kilometa 1445. Anaripoti Mwandisi Wetu, Kagera … (endelea).

Waziri Kalemani aliyasema hayo hivi karibuni mjini Bukoba nkoani Kagera wakati akifungua na kuongoza kongamano la wadau  kuhusu mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka nchini Uganda hadi Tanga Tanzania ambapo aliwaeleza wadau hao fursa mbalimbali za mradi huo na ni hatua gani mradi umefikia kabla ya kuanza kwasasa.
Waziri Kalemani alisema kwa kuwa Mkoa wa Kagera ndipo bomba la mafuta kutoka nchini Uganda litaaingilia Tanzania Wizara pamoja na wadau wa ujenzi wa mradi huo kwapamoja waliamua kukutana ili wananchi waelewe vizuri ni namna gani watanufaika na kwa sasa mradi upo katika hatua gani ili elimu iwafikie kule bomba litakapopita.
“Nimefurahishwa na utayari wa mkoa kwa namna mlivyochangia mawazo yenu unaweza kuona utayari wa kushiriki katika mradi huu mkubwa wa kimataifa, mradi huu unatarajia kuajiri watu 10,000 wakati wa ujenzi na watu 20,000 wakati ukikamilika lakini naona Kagera tayari mmeulewa mradi vizuri na kati ya ajira hizo lazima mhakikishe ajira na fursa za wazabuni mbalimbali zinabaki hapa,” alisena Kalemani.
Waziri Kalemani aliwahakikishaia wananchi  mkoani Kagera kuwa Serikali ya Tanzania na Serikali ya Uganda zimefikia asilimia 80% ya majadiliano ya utekelezaji wa mradi tangu kusainiwa mkataba wa makubaliano Mei 26, 2017 na mara baada ya majadiliano hayo kukamilika kwa asilimia 100% ujenzi wa bomba unatarajia kuanza Septemba 2019 na utekelezaji wa ujenzi  utakuwa tayari baada ya  miaka mitatu.
Vile vile Waziri Kalemani alisema kuwa wananchi waliotathminiwa mali zao kupisha bomba la mafuta  wataanza kupatiwa taarifa za tathmini zao watalipwa kiasi gani kuanzia wiki ya pili ya mwezi huu wa Juni 2019.
Na aliongeza kuwa jumla ya wananchi 10,000 walitathminiwa  katika mikoa minane na kwa mkoa wa Kagera ni wananchi 2017 ndiyo watapisha bomba la mafuta ghafi.
Kwa upande wake mratibu wa mradi huo taifa Salum Mnuna alisema bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga Tanzania utakuwa na urefu wa kilometa 1445 na asilimia 80% ya kilometa hizo zitakuwa upande wa Tanzania ambazo ni kilometa 1147 na asilimia 20% zinazobaki zitakuwa upande wa Uganda ambapo bomba hilo litapita katika mikoa minane ya Tanzania, Wilaya 24 na Kata 134.
Aidha aliitaja  Mikoa  nane ambayo ni Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma Manyara na Tanga aidha, katika Mkoa wa Kagera bomba litapita katika Wilaya za Missenyi, Bukoba (vijijini), Muleba na Biharamuro.
Mnuna alisema pia Bomba la mafuta ghafi litakuwa linasafirisha mapipa ya mafuta 216,000 kwa siku na kila pipa moja litakuwa linalipiwa kodi ya dola 12.5 za Kimarekani ukiachilia mbali na kodi nyinginezo zitakazokuwa zinalipwa kwa nchi nchi ya Tanzania.
Aidha aliongeza kuwa Makampuni makubwa matatu ndiyo yatateleza mradi huo nayo ni TOTAL kutoka Uingereza, TULLOW kutoka Ufaransa na CNOOC kutoka nchini China.
Aliongeza kuwa Katika mradi mzima wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi vitajengwa vituo sita vya kusukuma mafuta viwili upande wa Uganda na vinne upande wa Tanzania na  katika vituo vinne vitakavyojengwa Tanzania kituo kimoja kitajengwa Kyaka Wilayani Missenyi Mkoani Kagera, kingine kitajengwa mkoani Singida na viwili vitajengwa mkoani Tanga.
Katika hatua nyingine wananchi wa mkoa Kagera walishauri mradi kuzingatia kutoa kipaumbele kwa wazawa ili waweze kunufaika na mradi huo na usiwe kama miradi mingine inayoletwa nchini kukuta inatekelezwa na watu na wasio kuwa wazawa huku wazawa wakiwa na uwezo wa kufanya shughuli zinazokuwepo.
error: Content is protected !!