November 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Hussein: Kupata ushindi Z’bar ni ngumu

Maalim Seif Sharrif Hamad, Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo

Spread the love

KAZI ya kuutafuta ushindi kwenye uchaguzi mkuu visiwani Zanzibar ni ngumu. Anaripoti Hamis Mguta … (endelea).

Hiyo ni kauli ya Dk. Hussein Mwinyi, mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), aliyoitoa baada ya kuchaguliwa na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho leo tarehe 10 Julai 2020.

Kwenye uchaguzi huo, Dk. Mwinyi amechaguliwa kwa kura 129 (asilimia 78.65), Shamsi Vuai Nahodha akipata kura 16 (asilimia 9.76) na Dk. Khalid Salum Muhamed akipata kura 19 (asilimia 11.58).

          Soma zaidi:-

Dk. Mwinyi amewaeleza wajumbe wa NEC, kwamba kazi iliyoko mbele ni kubwa, lakini anaamini atafanikiwa kwa kuwa haitakuwa kazi ya peke yake, bali ya WanaCCM wote.

Dk. Hussein Mwinyi

“Lakini leo tumemaliza namshukuru Mungu huku nikijua kwamba kazi iliyokuwa mbele ni kubwa zaidi, lakini nafarijika kwamba haitakuwa yangu peke yangu ni yetu sote,” amesema Dk. Mwinyi.

Amesema, kinyang’anyiro cha uteuzi wa mgombea Urais wa Zanzibar, kilikuwa sawa na mtihani mkubwa kwake, lakini anamshukuru Mungu kwamba amefaulu.

“Zoezi hili halikuwa rahisi, mimi katika maisha yangu nimefanya mitihani mingi lakini mkubwa ulikuwa huu.  Mkiniona napungua ni kwa sababu hii,” amesema Dk. Mwinyi.

error: Content is protected !!