Thursday , 30 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Dk. Hoseah: Wakiniacha nitawashangaa
Habari MchanganyikoTangulizi

Dk. Hoseah: Wakiniacha nitawashangaa

Dk. Edward Hoseah, mgombea Urais TLS
Spread the love

 

DAKTARI Edward Hoseah, Mgombea Urais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), amesema atashangaa wanachama wa chama hicho wasipomchagua, kwani anawafaa katika nafasi hiyo kutokana na uzoefu wake kwenye uongozi .Anaripoti Regina Mkonde, Arusha … (endelea).

TLS itafanya uchaguzi Ijumaa tarehe 16 Aprili 2021 jijini Arusha, Dk. Hoseah atachuana na wagombea wengine wanne ambao ni; Flaviana Charles, Albert Msando, Shehzada Walli na Francis Stolla.

Akizungumza na MwanaHALISI Online leo Jumatano tarehe 14 Aprili 2021 jijini Arusha, Dk. Hoseah amesema, yeye ni mgombea pekee mwenye uzoefu, ikilinganishwa na wenzake ambao ameeaita kuwa ni wachanga

“Washindani wenzangu ni wazuri lakini ni wachanga. Tena kwa wakati huu wakiniacha nitawashangaa sana. Nina uzoefu na umahiri,” amesema Dk. Hoseah.

Dk. Hoseah amejinadi akisema, yeye ni mtu imara mwenye uwezo wa kupambana na dhoruba.

“Mimi ni mtu aliyepitia dhoruba. Kiongozi anatakiwa awe imara, mimi sitetereki kwenye dhoruba. Tena ndiyo nazipenda ili nifanye kazi zangu vizuri,” amesema Dk. Hoseah.

Akizungumzia kinyang’anyiro hicho, Dk. Hoseah amesema atashinda kiti chs urais.

“Mimi nitashinda labda zitumike mbinu chafu ambayo sidhani kama TLS ina mambo hayo,” amesema Dk. Hoseah.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NMB Bonge la Mpango – ‘Moto Uleule’ yazinduliwa, Milioni 180…

Spread the loveMSIMU wa tatu wa Kampeni ya kuhamasisha utamaduni wa Kuweka...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awataka wahariri kufanya kazi bila uoga, upendeleo

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amewataka wahariri wa vyombo...

Habari Mchanganyiko

STAMICO yasaini mkataba wa bilioni 55.2 kuchoronga miamba GGML

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limezidi kufanya vizuri katika...

Habari Mchanganyiko

NMB yatoa traksuti za Mwenge wa Uhuru Mtwara

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa traksuti kwa mkoa wa Mtwara ambako...

error: Content is protected !!