
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk. Edward Hoseah
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru),imewapelekea salamu nzito wagombea wa nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu kuachana na vitendo vya utoaji rushwa kwa kuwa walivyojipanga haitakuwa na nafasi. Anaandika Jimmy Mfuru … (endelea).
Aidha, wapiga kura wametakiwa kuacha kuuza utu wao kwa kuhongwa kanga na sukari haitawasidia chochote kwa kuwa watajikuta wakichagua wagombea wasiokuwa na sifa kwa kendekeza kuhongwa vitu vidogo.
Hawakuachwa mbali wagombea wa nafasi kwa kupewa angalizo kuwa matumizi ya fedha katika kipindi hicho cha chaguzi kutokiuka sheria mpya ya gharama za uchaguzi.
Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Dk.Edward Hoseah alipokuwa akizungumzia jinsi walivyojipanga kudhibiti rushwa katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika oktoba mwaka huu.
“Epukeni kutoa rushwa kwa wapiga kura wenu takukuru tumejipanga na rushwa kipindi hiki haitakuwa na nafasi na wapiga kura msiuze utu wenu kwa kuhongwa kanga na sukari”,amesema Dk.Hoseah
Aidha,amesema wamejipanga zaidi baada ya kupatiwa msaada wa vifaa vya shilingi bilioni tatu kutoka serikali ya watu wa China kwa ajili ya kuongeza ufanisi zaidi katika kupiga vita rushwa.
More Stories
Uholanzi, Uturuki ‘waingia’ vitani
Kuvunjwa kwa Jiji la Dar giza nene latanda
Ukomo wa urais uheshimiwe