May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Hoseah atakiwa kulinda heshima TLS

Dk. Rugemeleza Nshala, Rais wa TLS anayemaliza muda wake, akimkabidhi ofisi, Rais mpya, Dk. Edward Hoseah

Spread the love

 

DAKTARI Rugemeleza Nshala, Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika aliyemaliza muda wake, amemtaka mrithi wake, Dk. Edward Hoseah, ailinde heshima ya chama hicho, aliyoiacha. Anaripoti Regina Mkonde, Arusha … (endelea).

Dk. Nshala ametoa wito huo leo Jumamosi tarehe 17 Aprili 2021, wakati akiaga katika mkutano mkuu wa chama hicho, uliofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), jijini Arusha.

Rais huyo mstaafu wa TLS, amewaaga mawakili wa chama hicho, baada ya muda wake wa uongozi wa miaka mwili (Aprili 2019-Aprili 2021), kumalizika kufuatia uchaguzi mkuu uliofanyika Ijumaa tarehe 17 Aprili 2021 na kumuingiza madarakani Dk. Hoseah.

Akiaga katika mkutano huo, Dk. Nshala amesema, yeye na uongozi uliomaliza muda wake, wanaiacha TLS ikiwa imara, hali iliyothibitishwa na muitikio mkubwa ndani na nje ya nchi, kuufuatilia uchaguzi huo.

“Tumejitahidi kusukuma gurudumu hili tulipoweza, tumelinda heshima ya chama chetu kama mlivyoona jana, uchaguzi wetu umefuatiliwa na watu dunia nzima, hii inaonesha hiki si chama cha hovyo hovyo. Ni chama chenye heshima kubwa sana wanaokuja waendelee kuilinda,” amesema Dk Nshala, Rais TLS.

Dk. Nshala amewaahukuru wanachama wa TLS kwa kumchagua kuwa rais wao.

“Nashukuru tumeweza kufika mwisho wa uongozi wetu, mwisho wa siku tumefanya uchaguzi na kuimarisha demokrasia katika chama chetu.”

“Asanteni kwa heshima mliyotupa kuwaongoza, tuzidi kushikamana na kuwatakia kila la kheri, wanaokuja waweze kuliendeleza hili gurudumu mbele,” amesema Dk. Nshala.

Dk. Hoseah ataiongoza TLS kwa muda wa mwaka mmoja kuanzia Aprili 2021 hadi Aprili 2022.

error: Content is protected !!