December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Gwajima aziwekea kitanzi taasisi za afya

Spread the love

 

WAZIRI Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima ameziagiza taasisi za afya kufuata utaratibu wa mikataba ya utoaji huduma, ambayo inampa nafasi mteja kutoa madai yake iwapo taasisi hizo hazikidhi viwango na ubora wa huduma, zilizoainishwa katika mikataba hiyo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Dk. Gwajima ametoa agizo hilo leo Jumatatu, tarehe 25 Oktoba 2021, mkoani Dar es Salaam, akifungua mafunzo ya utoaji huduma bora kwa wateja, yaliyoandaliwa na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Waziri huyo wa afya, amesema utaratibu huo wa mikataba ya utoaji huduma ilianzishwa na Serikali 2001, ili kuziwezesha taasisi za afya nchini kutoa huduma bora kwa raia na wateja wa taasisi hizo.

“Mwaka 2001, Serikali iliona bora kuweka msingi wa kuziwezesha taasisi za umma, kutoa huduma bora kwa raia kwa kuanzisha utaratibu wa kutumia mikataba ya utoaji huduma kwa wateja. Ikiwa ni ahadi za kimaandishi zinazotolewa na taasisi kwa raia, au wateja wake kuhusu viwango na ubora wa huduma wanazotoa,” amesema Dk. na Dk. Gwajima.

Waziri huyo wa afya amesema “matarajio ya wananchi, ambayo raia anaweza kutoa madai yake endapo miadi iliyotolewa haijatekeleza inavyopaswa. Kwa hiyo Serikali 2001 ilianza habari za mkataba wa utoaji huduma kwa wateja.”

Jengo la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili

Dk. Gwajima ametoa agizo hilo, baada ya baadhi ya taasisi za afya kutofanyia kazi utaratibu huo uliowekwa miaka 20 iliyopita.

“ Leo 2021, miaka imepita 20 coverage ya hii mikataba ni asilimia ngapi? Leo tukifanya evaluation iko mingapi na inafanya kazi mingapi ipasavyo? Nadhani Muhimbili hilo mnatakiwa mlione, mlifanye sambamba na maono ambayo imeanzisha eneo hili hapa,” amesema Dk. Gwajima.

Dk. Gwajima amesema, utaratibu huo ukitumika ipasavyo itasaidia kuongeza imani ya wananchi katika huduma zinazotolewa na taasisi hizo, pamoja na kubainisha watumishi wake wasiotekeleza majukumu yao.

“Mikataba ya utoaji huduma kwa wateja ni mtaji wa mafanikio ya taasisi au ni mtaji wa mafanikio ya mtoa huduma hiyo, mmoja mmoja, kitengo au idara. Lakini ni mtaji wa kumfanya mteja kuwa na furaha, sababu ndani ya mkataba kama unaweka viwango vikifikiwa taasisi inatoka kwenye level moja kwenda nyingine,” amesema Dk. Gwajima .

Dk. Gwajima amesema “Na level hiyo ni ya kupendwa na wateja ya kutambulika na wale wateja watarudi kwako, kama viwango hujavifikia wale wateja watahama kwako wataenda kwa mwengine. Halafu wewe utabaki hapo huna wateja, matokeo ya kukosa wateja kila mtu anayajua, kwanza utageuka ni mfujaji wa mali ya Serikali unalipwa mshahara wa nini wakati kazi yako iko sifuri na wote wameshakukimbia.”

Akizungumza kuhusu mafunzo hayo, Dk. Gwajima amesema yamekuja katika wakati sahihi ambapo washiriki wake watapata mbinu za kutekeleza program iliyoanzishwa na Serikali 2000, ya kuboresha utumishi wa umma ili kuongeza ufanisi katika utoaji huduma za kuridhisha kwa wananchi.

error: Content is protected !!