Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Dk. Gwajima atoa maelekezo kwa maofisa maendeleo nchini
Habari Mchanganyiko

Dk. Gwajima atoa maelekezo kwa maofisa maendeleo nchini

Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto, Wazee na Makundi Maalum Dk.Dorothy Gwajima
Spread the love

 

WAZIRI wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto, Wazee na Makundi Maalum Dk.Dorothy Gwajima leo tarehe Mosi Juni 2023 amewaagiza  maafisa Maendeleo ya Jamii ,Ustawi wa Jamii jamii na Makatibu Tawala wasaidizi kuhakikisha wanafanya kazi zenye kuwa na tija katika kutelezela mpango wa Malezi na  makuzi ya awali ya maendeleo ya mtoto wa Tanzani. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea). 

Dk. Gwajima ametoa maelekezo hayo leo  wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya siku tatu ya utekelezaji wa mpango huo kwa nia ya kumlinda mtoto wa kitanzania mwenye kuanzia sikusufuri hadi miaka nane yanayofanyika kwa siku tatu jijini Dodoma kwa kuwashirikiasha kada hizo kutoka Mikoa 26 ya Tanzania bara.

Dk.Gwajima amesema  kuwa pamoja na nchi kuwa na uhuru kwa maana ya ukumbozi wa mipaka ya nchi lakini kada hizo kwa sasa zinatakiwa mkombozi zaidi kwa kuhakikisha watoto wanajengwa vyema kifikra ili kuweza kuwa na taifa lenye uwezo mkubwa wa kiakili ambalo pia litakuwa na wazalishaji wa kiuchumi kwa taifa na kimataifa.

“Dhana ya serikali ni kuhakikisha inawekeza kwa watoto wa siku 0 hadi miaka 8 na wanaotakiwa kufanya kazi hiyo ni  Maafisa Maendeleo ya Jamii ,Ustawi wa Jamii jamii na Makatibu Tawala wasaidizi kwa kuwa wanayo nafasi kubwa ya kuweza kuifikia jamii na kutoa elimu juu ya malezi na makuzi ya awali ya Mtoto wa Tanzania kwa lengo la kumlinda na masuala mazima ya unyanyasaji.

“Pamoja na mabo mengine mnatakiwa kufanya kazi kwa ubunifu kwa kuwafanya watu wengi kujua lengo hilo na kulipa umuhimu zaidi na pale mnapokuwa katika makundi ya mitandao ya kijamii ni lazima mhakikishe mnachombeza umuhimu wa kumlinda mtoto kwa nia ya kuelezea mpango wa PJT MMMAM ambao mlengo yake makubwa ni kuhakikisha analindwa mtoto na kupewa haki zake zote zamsingi” ameeleza Dk. Gwajima.

Katika hatua nyingine amewataka Maosifa Maendeleo kuonesha kazi zao kwa vitendo ili kuifanya jamii kuiga mambo yaliyomema na kuwatafuta mabalozi ambao watahakikisha wanapambana kuielimisha jamii jinsi ya umuhimu wa malezi na makuzi ya awali ya maendeleo ya mtoto wa Tanzania kwa nia ya kumfanya kila mmoja kubadilisha mawazo yake na kuwa na mawazo mapya juu ya malezi bora.

Aidha Dk. Gwajima amesema kuwa malezi na makuzi ya awali ya maendeleo ya Mtoto wa Tanzania ni ya kudumu na utakuwa na bajeti yake ambayo itawafanya watumishi wa kada mbalimbali ambazo zinahusika na malezi kujua bajeti yao na jambo hilo Rais Samia Suluhu Hasani kinara wa malezi analifanyia kazi kwa nguvu kubwa.

Naye Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Children in Crossfire Creig Ferla alisema kuwa iwapo watoto watapewa misingi bora na mizuri toka awali ni wazi kuwa taifa litakuwawatoto sahihi wenye kujitambua na wenye tija kubwa katika jamii.

“Watoto ni tunu ya taifa na wanabeba dira ya taifa na ifahamike kuwa watoto wenye umri kati ya siku 0 hadi nane ni asilimia 67 ya watanzania wote hivyo kati ya watu wazima nane kuna mtoto kati ya umri huo mmoja .

“Na kwa maana hiyo watoto wenye umri huo ni milioni 16 na kama watoo hao watapewa malezi na makuzi baora ya awali ni wazi kuwa watoto hao watakuwa bora zaidi kuliko watoto wengine ambao hawajapata malezi bora na hivyo watakuwa taifa lenye kuwa na tija.

“Watoto hao wakilelewa vema taifa litakuwa na uwezo wa uhakika wa kukuza uchumi wa nchi na taifa kwa ujumla wake taifa litaweza kujivunia kuwa na watu makini na wachapakazi na wenye kuwa na uelewa mpana na wa kutosha na hawawezi kuyumbishwa kwa jambo lolote” ameeleza Ferla.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!