May 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Gwajima ahimiza lishe bora, mazoezi

Spread the love

 

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima amewahimiza Watanzania kula lishe bora. Anaripoti Mwandishi Wetu, Katavi…(endelea).

Pia amewataka kufanya mazoezi ili kujikinga na magonjwa ikiwemo yanayisababisha changamoto ya upumuaji.

Dk. Gwajima ametoa wito huo Jumamosi tarehe 13 Machi 2021, katika mazoezi yaliyofanyika mkoani Katavi.

Unapofanya mazoezi na kula lishe bora unajiongezea kinga ya mwili na katika lishe epukeni kutumia chumvi na sukari nyingi na kunyweni maji ya kutosha na kupata muda wa kupumzika.

“Utaratibu huu utawezesha mwili wako uweze kujenga silaha bora zaidi ya kujikinga na magonjwa yasiyombukiza ikiwemo changamoto ya upumuaji” amesema Dk. Gwajima.

Wakati huo huo amewaagiza Waganga Wakuu wa Mikoa kuwaelimisha wananchi  madhara ya uzito uliopitiliza, sambamba na  kuweka utaratibu wa kuwapima uzito kulingana na urefu wao na kisha kiwashauri namna ya kupungua.

Pia, Dk. Gwajima amewaagiza wanganga wa tiba asili na mbadala kujisajili katika Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala.

Amewahimiza wananchi kutumia tiba za asili kukabiliana na magonjwa mbalimbali ikiwemo yasiyoambukiza.

error: Content is protected !!