June 17, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Dau sasa matatani

Spread the love

DK. Ramadhan Dau, aliyekuwa mkurugenzi wa Shirila la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote kutoka sasa. Anaandika Pendo Omary…(endelea).

Dk. Dau anatuhumiwa kuingiza NSSF hasara ya mabilioni ya shilingi, kutokana mikataba ya kinyonyaji. Amekuwa katika shirika hilo kwa miaka 15.

Taarifa kutoka serikalini na taasisi nyingine zinazoshughulikia uchunguzi zinasema, Dk. Dau ambaye aliong’olewa NSSF 15 Februari mwaka huu, atafikishwa kwa mahakamani, kujibu tuhuma za ufisadi zilizoibuliwa ndani ya shirika hilo.

Tuhuma nyingine ni matumizi mabaya ya madaraka, uzembe na ukiukwaji wa taratibu katika miradi ya uwekezaji na vitega uchumi mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Miongoni mwa miradi hiyo, ni ujenzi wa daraja la Kigamboni; hoteli ya kitalii jijini Mwanza, mradi wa ujenzi wa majengo katika mji mpya wa Kigamboni, uwekezaji kwenye jengo la biashara la Mzizima na mgodi wa mkaa wa mawe wa Kiwira, mkoani Mbeya.

Kwa habari zaidi, soma gazeti la MSETO kesho Alhamisi.

error: Content is protected !!