Monday , 11 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Bisimba wa LHRC ajivisha ‘mabomu’
Habari za Siasa

Dk. Bisimba wa LHRC ajivisha ‘mabomu’

Mkuregenzi Mtendaji wa LHRC, Dk Hellen Kijo -Bisimba
Spread the love

KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimejivisha mabomu na kukataa wazi wazi mpango wa serikali kilichodai kwamba ni muendelezo wa kuminya uhuru wa vyombo vya habari hapa nchini. Anaripoti Faki Sosi …. (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi mtendaji wa LHRC, Dk, Hellen Kijo Bisimba amesema kuwa vigezo vilivyotumiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuvipa adhabu vituo televisheni vinaashiria kuminya uhuru wa mawazo.

Kituo hicho kimetoa shutuma hizo kwa TCRA ikiwa ni siku moja tangu vituo hivyo vilivyopatiwa adhabu ya kulipishwa fedha kutokana na makosa yanayodaiwa kwamba yaliyokuwa yanaashiria uchochezi.

Vyombo hivyo vimepewa adhabu hiyo kutokana na kukiuka kanuni za utangazaji, kutangaza habari za uchochezi ambazo zimedaiwa zingehatarisha usalama wa taifa.

Alivitaja vituo hivyo kuwa ni pamoja na AZAM TV, ambacho kimelipa Sh. 7.5 milioni, Star TV ( Sh. 7.5 milioni), East Afrika TV ( Sh. 15 milioni) na Channel Ten ( Sh. 15 milioni)

Dk. Bisimba ameeleza kuwa TCRA imekiuka kifunga cha 18 cha katiba kutokana na kuminya uhuru wa mawazo na kujileza.

Ameeleza kuwa habari vimekosa uhuru wake wa kutoa taarifa kwa jamii husasani zile zinazoikosoa serikali moja kwa moja katika utekelezaji wa majukumu yake.

Ametoa mfano kuwa mwaka 2017, jamii imeshuhudia magazati mbalimbali yakifungwa na mengine kupewa onyo.

Amesema kuwa serikali kupitia Jeshi la Polisi imekuwa ikitumia neno uchochezi ili kuminya uhuru wa kijieleza na uhuru wa mawazo mpaka kwenye maeneo ya kijamii.

Akitoa mfano Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA ilijiingiza kwenye malumbao na Askofu, Zakaria Kakobe kutokana na mahubiri yake Kanisani bila sababu ya msingi.

Amesema kuwa kiashiria kingine cha kuminywa kwa uhuru wa maoni ni pamoja na kukamatwa kwa wanasiasa waliokosoa serikali kutokana utendaji wake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Jaji Kiongozi akerwa wananchi kukosa imani na mahakama

Spread the loveWATENDAJI wa Mahakama ya Tanzania, wametakiwa kuweka mikakati itakayosaidia kurejesha...

BurudikaHabari za Siasa

Samia amchangia Professa Jay mil. 50, Chadema, wasanii wamwaga manoti

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amechangia kiasi cha Sh 50 milioni...

Habari za Siasa

Biteko: Samia ni muumini wa maridhiano sio kwa kuigiza

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Mpango: Sitakufa bali nitaishi

Spread the loveMAKAMU  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk....

error: Content is protected !!