Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Bashiru: Nilipata taarifa za uteuzi mitandaoni
Habari za SiasaTangulizi

Dk. Bashiru: Nilipata taarifa za uteuzi mitandaoni

Dk. Bashiru Ally
Spread the love

 

DAKTARI Bashiru Ally, Katibu Mkuu Kiongozi amesema, taarifa za kuteuliwa kwake, kwa mara ya kwanza alizipata kupitia mitandaoni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Ametoa kauli hiyo leo tarehe 27 Februari 2021, wakati akiapishwa kushika wadhifa huo Ikulu, jijini Dar es Salaam.

“Jana jioni niko nasoma mafaili yangu, napata taarifa kupitia kwenye mitandao kwamba umeniteua.

“Mshtuko huo hauniwezeshi niseme, bado natafakari sana nitafanya nini, nifanye nini kukidhi maratajio yako kwa imani uliyonipa mfululizo,” Dk. Bashiru alimueleza Rais John Magufuli.

Rais John Magufuli

Pia amemshukuru Rais Magufuli kwa kumwamini huku akimuahidi, kuwa hatomuangusha katika nafasi hiyo aliyomteua.

“Nakushukuru kwa imani yako kubwa, hii ni mara ya pili kwa kunipa wadhifa mkubwa; kwanza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na sasa utendaji ndani ya serikali, imani hiyo nitailipa kwa imani,” amesema Dk. Bashiru.

Dk. Bashiru aliteuliwa jana kushika wadhifa huo uliokuwa umeshikiliwa na Balozi John Kijazi, aliyefariki dunia tarehe 17 Februari 2021. Kabla ya uteuzi huo, Dk. Bashiru alikuwa Katibu Mkuu wa CCM.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!