December 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Bashiru: Kamateni hao CCM

Dk. Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa CCM

Spread the love

KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally amesema, mgombea yeyote wa chama hicho atakayejihusisha na vitendo vya rushwa, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wamkamate. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza na wanachama wa chama hicho tawala katika Mji wa Kibaya, Kiteto mkoani Mara leo tarehe 12 Julai 2019 amesema, rushwa haikubaliki kwenye chama hicho na kwamba, anayekamatwa sheria ichukue mkondo wake.

Dk. Bashiru yupo mkoani Manyara kwa ziara ya siku mbili ambapo amesema, CCM haikubaliani na viongozi watakaopatikana kwa nununua uongozi.

Na kwamba, uchaguzi wa serikali za mtaa baadaye mwaka huu, hatarajii chama hicho kiwe na viongozi waliopatikana kwa rushwa.

Amesisitiza kwamba, viongozi wanaotarajiwa kupatikana kwenye uchaguzi huo, wanapaswa kutokana na uadilifu wao wenyewe na si kubebwa.

error: Content is protected !!