Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Bashiru: CCM kuna wezi
Habari za SiasaTangulizi

Dk. Bashiru: CCM kuna wezi

Spread the love

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Bashiru Ally amesema kuwa, ndani ya chama chake amekuta wezi. Anaandika Faki Sosi…(endelea).

Na kwamba, kuna wabunge kwenye chama chake wanapochangia mijadala bungeni unaweza kudhani wazalendo lakini wezi.

Dk. Bashiru ametoa kauli hiyo leo tarehe 12 Oktoba 2018 wakati wa Kongamano la Miaka 19 ya Kumbumbuku ya Mwalimu Nyerere lililopewa mada ya Mienendo ya Chaguzi na Mustakabali wa Mataifa Afrika ambalo limefanyika kwenye Ukumbi wa Nkurumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Amesema kuwa, ni miongoni mwa mambo aliyoyakuta ndani ya CCM na kuanza kukabiliana nayo. Jambo lingine ni kutokuwepo kwa mtazamo mtazamo wa pamoja.

Amesema kuwa, kuna mbunge wa chama hicho alimkuta na gari ya chama aliyoichukua na kuitumia kwa maslahi yake, alikabiliana naye hapohapo na kumtaka ashuke.

“Tena kuna mbunge mmoja nilimkuta kwenye gari, nikamwambia ashuke hapohapo la sivyo nitamkamata hata kwa polisi,” amesema na kungeza;

“Ukimtazama unavyoongea bungeni unaweza kudhani kama ni mzalendo lakini ni mwizi.”

Dk. Bashiru alikuwa akieleza namna alivyokabiliana na baadhi ya mambo yasiyopendeza kwenye chama hicho. Ni wakati ambao alikuwa kwenye tume ya kukihakikia mali za chama hicho.

Akizungumza kwenye kongamano hilo Dk. Bashiru amesema kuwa, vyama vyote vinapaswa kuwa na vyanzo vya mapato ili kuweza kujisimamia na kuepuka kuendeshwa na watu wa mataifa ya nje.

Kwenye kongamano hilo ameeleza madhara ya chama kutokuwa na uwezo wa kifedha katika kupanga na kujiendesha kwenye shughuli zake.

Amesema kuwa, vyama vinapaswa kuwa na uwezo wa kifedha ili kuepuka kutekwa na matajiri ambao watakuwa ndio wapangaji wa mambo na uongozi.

“Bila chama kuwa na mitaji yake tutapotea. Tuache watu wa nje kuja kuendesha vyama vyetu. Wafukuzeni matajiri wanaokuja kupanga uongozi,” amesema na kuonya kuwa, ni hatari zaidi pale mataifa ya nje yatakapokuwa wafadhili wakubwa wa vyama hivyo.

Hata hivyo amesema kuwa, changuzi zijazo anakwenda kushinda licha ya wapinzani kulalamika kuwa, CCM inanunua wapinzani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

error: Content is protected !!