Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Bashiru apiga mkwara Z’bar
Habari za Siasa

Dk. Bashiru apiga mkwara Z’bar

Dk. Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa CCM
Spread the love

KAULI iliyowahi kutolewa na Humphry Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM visiwani Zanzibar mwaka jana kwamba, kambi hazitasidia kupata mgombea, leo tarehe 3 Novemba 2019, imetolewa na Dk. Bashiru Ally. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).  

Akiwa Pemba, Dk. Bashiru amezungumza kwenye kamati ya siasa Wilaya ya Chakechake, kwamba mikakati yao ya kutaka kupitishwa ili kugombea udiwani, ubunge na hata urais, inakiuka miiko ya chama hicho.

Dk. Bashiru yupo ziarani visiwani humo, ambapo amekuwa akikutana na viongozi mbalimbali pamoja na wanachama wa chama hicho.

Akizungumza Chadekchake Dk. Bashiru amesema, tayari ana taarifa kuhusu kuwepo kwa hekaheka za baadhi ya wanachama wao wakilenga kuteuliwa kugombea nafasi mbalimbali.

Mwaka jana, akiwa ziarani Zanzibar, Poleple aliwaonya wanachama wa visiwa hivyo kwamba, wanaojipitisha na kupanga mikakati ya kumrithi Dk. Mohammed Shein, rais wa sasa visiwani humo, wanajihangaisha.

Alisema, hakuna anayemfahamu mrithi wa Dk. Shein na wasidhani atapatikana kwa utaratibu waliouzoea. “Mimi niwaambie msijisumbue! chama kitamtoa “mtu wake” Dodoma; mtaletewa mumpigie kura huyo.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

error: Content is protected !!