May 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Bashiru akaa Ikulu siku 32, apewa ubunge

Spread the love

 

DAKTARI Bashiru Ally, aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, amehudumu nafasi hiyo nyeti ndani ya Ikulu ya Tanzania kwa siku 32. Anaripoti Matrida Peter, Dar es Salaam … (endelea).

Dk. Bashiru, amekaa Ikulu kuanzia tarehe 27 Februari 2021, siku aliyoapishwa kuwa Balozi na Katibu Mkuu Kiongozi na aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Pombe Joseph Magufuli.

Dk. Bashiru, aliapishwa baada ya kuteuliwa tarehe 26 Machi 2021 kushika nyadhifa hizo, ukiwa ni uteuzi na uapisho wa mwisho kufanywa na Dk. Magufuli kuufanya kabla ya kufikwa na mauti.

Aliapishwa kushika wadhifa huo, baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, kufariki dunia tarehe 17 Februari 2021, katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodoma.

Dk. Magufuli, aliyekuwa Rais wa Tanzania kuanzia tarehe 5 Novemba 2015 hadi saa 12:00 jioni ya Jumatano tarehe 17 Machi 2021, alipofikwa na mauti katika Hospitali ya Mzena, Dar es Salaam.

Mwili wa Dk. Magufuli ulizikwa nyumbani kwao, Chato mkoani Geita.

Safari ya utumishi wa Dk. Bashiru kwenye nafasi ya Katibu Mkuu Kiongozi, imehitimishwa leo Jumanne tarehe 31 Machi 2021, ikiwa ni siku 32, baada ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kumteua kuwa mbunge.

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania, Dk. Bashiru Ally

Baada ya kumteua kuwa mbunge, Rais Samia, amemteua Balozi Hussein Kattanga kuwa Katibu Mkuu Kiongozi.

Kabla ya uteuzi huo, Katanga alikuwa ni Balozi wa Tanzania nchini Japan.

Dk. Bashiru aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, akiwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi aliyokuwa ameihudumu kwa kipindi cha miaka miwili na miezi nane.

Dk. Bashiru Ally

Alipendekezwa na Dk. Magufuli tarehe 29 Mei 2018 na kuthibitishwa na wajumbe wa halmashauri kuu, iliyokutana Ikulu ya Dar es Salaam.

Aliteuliwa kushika nafasi hiyo ya katibu mkuu wa CCM, akiwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kuchukua nafasi ya Abdulrahman Kinana aliyekuwa amestaafu.

error: Content is protected !!