Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Bashiru aivimbia CCM
Habari za SiasaTangulizi

Dk. Bashiru aivimbia CCM

Spread the love

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Bashiru Ally, amepingana utamaduni ulioanza kujengwa ndani ya chama wa kupachika majina ya wagombea kwenye mashina mapya yanayofunguliwa. Anaripoti Hamis Mguta…(endelea).

Kiongozi huyo wa CCM amesema, majina ya mashina yanapaswa kubeba majina yenye ujumbe wa chama na serikali na si watu kama inavyojengeka sasa.

“Yanatakiwa majina yenye kubeba ujumbe wa chama na serikali,” amesema Dk. Bashiru na kuongeza “na sio majina ya wagombea.”

Dk. Bashiru ametoa kauli hiyo leo tarehe 1 Septemba 2019, akiwa kwenye ziara yake ya kichama katika jimbo la Kawe linaloongozwa na Halima Mdee wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Dk Bashiru alikuwa akizindua shina la Hapa Kazi Tu katika Kata ya Kawe, Dar es Salaam ambapo jina hilo ndio kauli mbiu ya Rais John Magufuli kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Katibu huyo wa CCM amekuwa akifanya ziara ya kuimarisha chama hicho huku kukiwa na malalamiko kutoka upinzani kwamba, Jeshi la Polisi linapendelea chama tawala huku upinzani ukinyimwa fursa hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!