May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Abbas aitaka Cosota kuwabana ‘wanaomnyonya’ Mb Dogg

Spread the love

 

WIZARA ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania, imeiagiza Taasisi ya Hakimiliki nchini humo (COSOTA), kufuatilia na kuhakikisha msanii Mb Dogg anapata haki zake kutoka kampuni ambazo zimetumia kazi zake bila yeye kupata chochote. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Agizo hilo, limetolewa jana Alhamisi tarehe 22 Julai 2021, jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk. Hassan Abbasi, alipomwita msanii huyo aliyekuwa amelalamika kwenye mitandao ya kijamii akiomba msaada wa kupiganiwa haki zake.

“Hili limeisha, COSOTA simamieni msanii huyu apate haki zake kutoka kampuni za ZIIKI na kampuni nyingine iitwayo ZEZE ambayo iko Kenya,” alisema Dk. Abbas na kuongeza:

“Mtawasiliana mara moja na wenzetu wa Kenya kuhakikisha kazi za Mb Dogg zinapata stahiki yake.”

Dk. Abbasi pia ameitaka COSOTA kuendelea kuweka kanuni zinazowalinda wasanii wa nchini huku akisisitiza uwazi katika makampuni yanayouza kazi za muziki

Kwa upande wake, Mb Dogg alisema, amekuwa katika juhudi za kurejea kimuziki lakini alishangazwa na kubaini kuwa nyimbo zake nyingi zinatumika katika mitandao ya kuuza muziki bila aidha makubaliano au pale penye makubaliano bila kupewa stahiki zake.

Pia, ameishukuru Serikali kwa kuingilia kati swala hilo na anaamini kupitia Serikali kwa sasa anaweza kupata haki yake.

error: Content is protected !!