Tuesday , 21 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Diwani wa Chadema aliyeuwawa atunukiwa tuzo
Habari za Siasa

Diwani wa Chadema aliyeuwawa atunukiwa tuzo

Godfrey Luena, enzi za uhai wake
Spread the love

ALIYEKUWA Diwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), katika Kata ya Namwawala, jimbo la Mlimba, mkoani Morogoro, Godfrey Luena, ametunukiwa “Tuzo ya Haki za Binadamu ya Majimaji,” kwa mwaka 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Luena ambaye alifariki dunia kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana, Februari mwaka 2018, alitunukiwa tuzo hiyo na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), wakati wa maadhimisho ya siku ya Haki za Binadamu duniani, juzi Alhamisi jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa ya LHRC iliyotolewa leo Jumamosi, tarehe 12 Desemba 2020, marehemu Luena ametunukiwa tuzo hiyo, kufuatia kujitoa kwake katika utetezi wa haki za binadamu enzi za uhai wake.

“Hayati Luena ametunukiwa tuzo hiyo kutokana na mchango wake mkubwa katika kusimamia haki za wananchi wa mkoa wa Morogoro hasa wilaya ya Kilombero, Ifakara na Ulanga,” imeeleza taarifa hiyo.

            Soma zaidi:-

Taarifa imesema, katika kipindi cha uhai wake, Lueana alijitoa bila kujali vitisho na maslahi yake binafsi, kutetea haki za wananchi waliodhulumiwa haki ya kumiliki ardhi na walioonewa na mamlaka kwa kusingiziwa makosa na kunyimwa haki ya dhamana.”

Marehemu Luena, alishinda tuzo hiyo baada ya kuwashinda wanaharakati wengine wa haki za bianadamu 32, waliopendekezwa kuwania tuzo hiyo, akiwemo mchora katuni mashuhuri, Ally Masoud (Kipanya) na aliyewahi kuwa Rais wa chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Fatma Karume.

Wengine walioshiriki shindano la kumpata mshindi, ni Roby Samwely na mwandishi wa habari na mtangazaji wa siku nyingi, Vicky Ntetema.

Tuzo hiyo inayotolewa mara moja kila baada ya miaka mitano, ilitolewa chini ya jopo la majaji lililoongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Mstaafu wa LHRC, Dk. Helen Kijo-Bisimba.

Dk. Helen Kijo Bisimba

Wengine waliokuwamo kwenye jopo la kutafuta mshindi, ni mwandishi wa habari mkongwe, Jenerali Ulimwengu na aliyepata kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na mtetezi wa Haki za Binadamu, Tom Bahame Nyanduga.

Mwingine aliyeshiriki katika kutafuta mshindi wa tunzo hiyo, ni Askofu Mkuu wa  Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Karagwe, Dk. Benson Bagonza.

LHRC imeutaja mchango wa Luena katika kutetea haki za wananchi wa mkoa wa Morogoro, ikiwemo kulinda haki za ardhi za wanakijiji waliopo kwenye vijiji vya pembezoni mwa Bonde la Kilombero (Ramsar).

Kwa mujibu wa LHRC, Lueana alisaida kufungua kesi dhidi ya wizara ya maliasili na Utalii, mwaka 2015, iliyosajiliwa Mahakama Kuu, Kitengo cha Ardhi na kupewa N. 161 ya mwaka 2015.

Katika kesi hiyo, Mahakama iliamuru Serikali ipitie upya mipaka ya bonde hilo na maamuzi hayo yalinufaisha asilimia 65 ya wananchi waishio katika vijiji hivyo.

“Akishirikiana na wenzake wawili, aliwatetea wananchi wa kijiji cha Chita katika mgogoro wao wa ardhi dhidi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Chita,” inaeleza taarifa ya kituo hicho cha sheria na kuongeza, “mgogoro huu, ulitatuliwa kwa usuluhishi na Chita JKT, wakaridhia kuachia wananchi wa eneo hilo, ekari 1600 za ardhi.”

Luena alifariki dunia usiku wa kuamkia tarehe 23 Februari mwaka 2018, akiwa nyumbani kwake, huko Mlimba. Mpaka sasa, haijaweza kufahamika, sababu hasa za utekelezaji wa mauwaji hayo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!