Diwani wa Kata ya Nsalaga jijini Mbeya, Mchungaji David Ngogo amesema ameamua kujiuzuru uanachama wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini ili kuondoka malumbana na viongozi wa Chadema.
Amesema amechukua uamuzi huo baada ya kutofautiana na viongozi wa Chadema kuhusu suala la maendeleo, ikiwa ni pamoja na uamuzi wake wa kumuomba Naibu Spika, Dk Tulia Ackson kusaidia maendeleo katika sekta ya elimu katika kata yake.
Wakati Ngogo akichukua uamuzi huo, leo uongozi wa chama hicho mkoani Mbeya umependekeza madiwani watatu wa jijini humo kufukuzwa uanachama kwa utovu wa nidhamu na kukiuka taratibu za chama, wakidaiwa kushiriki katika sherehe waliyoalikwa na Dk. Tulia mjini Dodoma.
Madiwani hao na kata zao kwenye mabano ni Geofrey Kajigili (Sisimba), Hamphrey Ngalawa (Iwambi) na Newton Mwatujobe (Manga).
“Yule (Dk Tulia) ni kiongozi na amekuwa akijitoa kusaidia jamii na sio Mbeya tu hata mikoa mingine. Hivyo na mimi nikamuomba afanye hivyo katika shule iliyopo katika kata yangu. Kweli alifanya hivyo na Alhamisi wiki hii alikuja pale akatoa msaada wa bati 100 na mufuko ya saruji,” amesema.
“Lakini katika hafla ya kupokea msaada ule niliwaona viongozi wengine lakini sikuwaona viongozi wanaotokana na Chadema.”
Amesema baada ya hafla hiyo ilianza kupokea simu kutoka kwa viongozi wa Chadema wakimlaumu kwa kitendo chake cha kumualika Dk. Tulia kwenda katika kata yake.
“Ukiona unapingana na kiongozi basi busara zikuongoze kwa kujiweka kando ili kila mmoja abaki na msimamo wake, ndio nilichokifanya,” amesema.
“Unapingana na viongozi wako halafu mwaka 2020 utasimama jukwaani kuwaambia wananchi kwamba hukuwaletea maendeleo kwa sababu viongozi wako hawapendi kuona wageni wanaleta maendeleo? Au utawaambia sikuwaletea maendeleo kwa sababu sikuwa na uhusiano mzuri na viongozi wangu? Watanielewa kweli.”
Spread the love RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...
By Mwandishi WetuMarch 20, 2023Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...
By Mwandishi WetuMarch 16, 2023Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...
By Mwandishi WetuMarch 15, 2023Spread the love KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...
By Mwandishi WetuMarch 14, 2023
Leave a comment