March 3, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Diwani Chadema auwawa kwa kukatwa mapanga

Godfrey Luena, enzi za uhai wake

Spread the love

DIWANI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kata ya Namwawala, Jimbo la Mlimba mkoani Morogoro, Godfrey Luena ameuawa usiku huu nyumbani kwake baada ya kushambuliwa kwa kukatwakatwa kwa mapanga na watu wasiojulikana. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Taarifa za awali zinasema muda mchache kabla ya kushambuliwa umeme ulikatika katika nyumba yake, ndipo alipolazimika kutoka nje ili kuangalia maana nyumba za jirani ulikuwa unawaka.

Alipozunguka nyuma ya nyumba yake kukagua tatizo ni nini ndipo alipokutana na kikosi cha watu wenye mapanga wakamkatakata hadi wakamtoa roho.

Joseph Haule, Mbunge wa Mikumi (Chadema) amethibitisha kutokea kwa kifo hicho kupitia ukurasa wake wa Twitter.

error: Content is protected !!