October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Diwani CCM kupigwa risasi: Viongozi Chadema wanaswa

Spread the love

VIONGOZI wawili wa Chadema, mkoani Songwe wameachwa huru, huku wawili wakifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Songwe, kwa tuhuma za kujaribu kumuua kwa risasi Diwani wa CCM. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Viongozi walioachwa huru ni Isakwisa Lupembe, Mwenyekiti wa Chadema mkoani Songwe na Joel Silungwe, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA) pamoja na mwanachama wa chama hicho, Kisigo Mwakabanje.

Waliofikishwa mahakamani ni Boniface Mwakabanje, Mwenyekiti Chadema Jimbo la Tunduma na Hamza Mponjolela, Mtunza Hazina wa Chadema.

Akizungumza na MwanaHALISI ONLINE jana tarehe 28 Novemba 2019, Boniface Mwabukusi, wakili anayewatetea viongozi hao, amesema watuhumiwa hao wamelifikishwa mahakani kwa kosa la kujaribu kuuwa kwa silaha.

Mwabukusi amesema, kwa sasa anashughulikia dhamana ya viongozi hao wa Chadema, katika Mahakama ya Rufaa ya Mbeya.

Mwakabanje na Mponjolela walikamatwa na polisi tarehe 23 Novemba 2019 wakituhumiwa kumjeruhi kwa risasi, Julius Mwavilenga, Diwani wa Kata ya Sogea (CCM).

error: Content is protected !!