May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Diwani CCM Dar afariki dunia, kuzikwa Kisarawe

Marehemu Karimu Madenge

Spread the love

 

DIWANI wa Buyuni (CCM), Wilaya ya Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam, Karimu Madenge amefariki dunia jana Jumatano, tarehe 4 Agosti 2021, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Amana jijini Dar es Salaam baada ya kuumwa kwa muda mfupi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mwenezi wa chama hicho, Wilaya ya Ilala, Said Sidde amesema, Madenge atazikwa leo Alhamisi kijijini kwao Kibuta, Kisarawe mkoani Pwani.

Kabla ya mwili wa Madenge kupelekwa kuzikwa, taratibi zingine zitaanzia nyumbani kwake Buyuni jirani na ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Sidde aliwataka wanachama wa chama hicho, kushiriki katika msiba huo ikiwemo kuchukua tahadhari ya kuvaa barakoa kwa ajili ya kujikinga na corona.

error: Content is protected !!