January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Diwani awashukuru wapiga kura, ailaumu NEC

Spread the love

ALIYEKUWA mgombea udiwani Kata ya Makurumla kwa tiketi ya CUF, Omary Thabit maalufu kwa jina la ‘Kijiko’ ametoa shukrani kwa wananchi walioshiriki kumpigia kura na kumfanya kuwa diwani wa kata hiyo kwa mwaka huu. Anaaandika Hamisi Mguta … (endelea).

Akizungumza na mwanaHALISI Online Thabit amesema jitihada za wananchi ndizo zilizomfanya kuwa mshindi wa udiwani katika kata hiyo kwa kumtoa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rajabu Hassan, ambaye alikuwa akitetea nafasi hiyo.

Thabit amekuwa diwani wa kata hiyo kwa mara ya kwanza akitokea chama cha upinzani baada ya kumshinda mgombea huyo wa CCM kwa kuwa na kura 12, 797 huku mgombea huyo akiwa na kura 10,143

Wagombea wengine aliokuwa akipambana nao ni Silvester Ruben kutoka ACT-Wazalendo, Khadija Jabir wa Chama Umoja na Maendeleo (CHAUMA), Issa Omary wa Tanzania Labour Party (TLP), Salima Khalfan, (JAHAZI ASILIIA) pamoja Neema Kasim wa UMD.

Katika kuwapongeza wananchi kwa ushindi waliompa anasema atahakikisha anawapa huduma zote alizoweka katika vipaumbele vyake kwasababu wananchi wanataka mabadiliko “nimefurahi sana kupata ushindi na nimefurahi pia kuona wananchi wakihitaji mabadiliko hadi kunichagua mimi kwani wasingetaka mabadiliko wasingenichagua, hivyo nitawatumikia ipasavyo”

Akizungumzia ushindi wa aliyekuwa mgombea wa CCM, Dk John Magufuli Thabit Anasema watu wengi walikua wakisubiri kuona jinsi Tume ya Taifa ya uchaguzi itafanyake kazi na kuwa huru katika utoaji wa matokeo kutokana na mivutano kadhaa iliyojitokeza kati ya chama tawala na vyama pinzani, kwa maana hiyo basi tume haikuwa huru katika utoaji wa matokeo na imeonekana kukibeba chama kimoja.

Amesema kwa kuwa CCM haiwezi kukubali kutoka madarakani imefanya kila njia kuhakikisha wanaingia madarakani na huenda wakawa wametekeleza ile ahadi yao ya kushinda kwa ‘goli la mkono’ “cha kushangaza zaidi ni ule ucheleweshaji wa matokeo kwa majimbo mbalimbali waliyoshinda wapinzani, hata matokeo ya Urais sijayaamini.

error: Content is protected !!