Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Diwani apiga marufuku uingizwaji wa taka sokoni
Habari Mchanganyiko

Diwani apiga marufuku uingizwaji wa taka sokoni

Spread the love

DIWANI wa kata ya Chamwino, jijini Dodoma, Jumanne Ngede amepiga marufuku uingizwaji wa taka za vifungashio vinavyoletwa na bidhaa mbalimbali kwenye dampo la soko la Bonanza, zinazozalishwa na wafanyabishara wa kutoka nje. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Vifungashio hivyo vilivyozuuliwa kwenye dampo hilo la soko ni vile vinavyoletwa huku vikiwa vimefungashiwa kwenye matunda ikiwemo ndizi, miwa, nyanya, machungwa na mahindi mabichi.

Ngede amepiga marufuku hiyo ya zuio la vifungashio wakati alipokuwa akizungumza na viongozi wa soko hilo la Bonanza jijini Dodoma, kwenye kikao cha kujadili uondoshwaji wa taka hizo zinazoletwa na wafanyabishara wa kutoka nje.

Alisema kwa mujibu wa sheria ya halmashauri ya jiji wale wote watakaobainika kutupa taka hizo kwenye dampo soko faini inazotonzwa ni kuanzia kiasi cha Sh. 50,000 hadi 300,000.

Alisema faini hizo zimewekwa kwa wale watakaobainika na kukiuka katazo hilo la kuzitupa taka hizo kwenye dampo hilo ikiwemo na makosa menginyo kwa mujibu wa kanuni na sheria.

Hata hivyo alisema kuwa vifungashio hivyo kwa wafanyabiashara hao wanatakiwa wanapoleta biashara zao kuondokanazo na kupeleka kwenye dampo lililotegwa lililopo Chidaya ambalo lipo kwa ajili ya kuhifadhi taka ambalo ni la kisasa.

“Lengo la jiji ni kuona mji wake unakuwa katika mazingira safi na haulemewi na wingi wa taka zozote za kutoka nje kwa kuwa wao hawahusiki,hivyo ninawaagiza nyinyi viongozi wa soko hili la Bonanza wafanyabishara hao wanaoleta bidhaa kuzingatia sheria na kanuni na wakikiuka wachukulieni sheria kali ikiwa na kulipa faini.”alisema.

Diwani huyo pia amewataka wafanyabishara na viongozi kuunda kikosi ambacho kitakachohakikisha dampo hilo halitumiki kwa kutupa taka za vifungashio na pindi wanapoona taka hizo zikitupwa kwenye eneo hilo wahusika wachukuliwa hatua za kisheria.

Kwa upande wake Afisa masoko wa jiji la Dodoma James Yuna alisema kuwa Halmashauri ya jiji tayari imeshatoa maelekezo ya kuwataka wafanyabiashara wote wanaoleta bidhaa zao zikiwa kwenye vifungashio wanaotokanazo.

Aidha ili waweze kudhibiti hali hiyo pia kwa wafanyabishara wenyewe wanatakiwa kutoa ushirikiana na halmashauri ya jiji ili kudhibiti hali hiyo ndani ya masoko yote ambayo tayari yameshapewa maelekezo ya kutotupa vifungashio hivyo.

Pia amewataka wafanyabiashara ndani ya masoko yote ya jiji kuhakikisha wanazingatia usafi wa mazingira wanayofanyia kazi badala ya kusubiri kufanyiwa na watu wengine hii ni pamoja na kuepukana na kufanya bishara kwenye maeneo yasiyo rafiki kwao na wateja wanaowahudumia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!