TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imetangaza kwamba, maombi ya kujiunga na vyuo vikuu kwa shahada ya kwanza katika mwaka wa masomo wa 2019/20, yataanza rasmi tarehe 15 Julai 2019. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Taarifa hiyo imetolewa leo tarehe 13 Julai 2019 na Profesa Charles Kihampa, Katibu Mtendaji TCU.
Prof. Kihampa amewataka wenye sifa za kudahiliwa kusoma kwa makini, vigezo vilivyo orodheshwa katika kitabu cha muongozo wa program zilizoanishwa na TCU, wathibitishe kama wana sifa stahiki za udahili zilizoainishwa na tume hiyo.
Pia, Prof. Kihampa amewataka waombaji wenye vyeti vilivyotolewa nje ya nchi kuviwasilisha vyeti vyao Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) au Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), ili kupata ithibati ya ulinganifu wa sifa zao kabla ya kuanza kuomba udahili.
Aidha, Prof. Kihampa amewataka wananchi kuwa makini na watu wanaojiita mawakala au washauri wa namna ya kujiunga na vyuo vya elimu ya juu hapa nchini.
Leave a comment