May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dilunga aondolewa kikosini Stars, Mudathiri ajumuishwa

Hassani Dilunga, kiungo wa Simba SC

Spread the love

KIUNGO wa klabu ya Simba Hassan Dilunga ameondolewa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) mara baada ya jina lake kutanjwa kimakosa huku wakati huo huo kiungo wa klabu ya Azam FC Mudathir Yahya akijumuisha kwenye kikosi hiko mara baada ya kutokuwepo kwenye orodha ya awali. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Kikosi hiko cha wachezaji 27, kimetangazwa hii leo na kocha mkuu wa Taifa Stars Kim Poulsen ambacho kitaingia kambini tarehe 5 Juni, 2021 kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Malawi.

Muda mfupi baada ya tukio hilo Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) lilitoa taarifa ya ufafanuzi ambayo ilieleza kuwa katika kikosi kilichotolewa kwa maandishi kilionesha mchezaji Hassani Dilunga ameitwa ikiwa ni kimakosa ya uandishi.

Aidha katika wakati huo huo taarifa hiyo ikaeleza kuwa kiungo wa klabu ya Azam FC Mudathir Yahya ameitwa kwenye timu hiyo licha ya jina lake kutonekana kwenye orodha ya awali.

Kikosi kamili hiko hapo chini.

error: Content is protected !!