Tuesday , 23 April 2024
Home Habari Mchanganyiko DIASPORA wamtwisha Kibatala zigo la uraia pacha, watinga mahakamani
Habari MchanganyikoTangulizi

DIASPORA wamtwisha Kibatala zigo la uraia pacha, watinga mahakamani

Wakili Kibatala
Spread the love

WATANZANIA sita waishio nje ya nchi (DIASPORA), wamefungua kesi ya kikatiba Na. 18/2022 katika Mahakama Kuu, Masjala Kuu, ya Dar es Salaam, kupinga vifungu vya sheria vinavyozuia uraia pacha, wakidai ni batili kwa kuwa vinakiuka haki yao ya kikatiba ya kuwa raia wa kuzaliwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Taarifa kuhusu kesi hiyo imetolewa leo Ijumaa, tarehe 16 Desemba 2022 na Wakili wa watanzania hao, Peter Kibatala, ambaye amesema imepangwa kutajwa kwa mara ya kwanza tarehe 20 Februari 2023, mbele ya Jopo la Majaji Watatu wa Mahakama Kuu, Jaji Mustafa Kambona Ismail, Jaji Obadia Festo Bwegoge na Jaji Hamidu Rajab Mwanga.

Watanzania hao, Shabani Fundi, Patrick Nhigula na Emmanuel C. Emmanuel, waishio nchini Marekani; Restituta Kalemera na Nkole Muya, waishio nchini Uingereza; pamoja na Bashir Kassam, aishiye Canada, wamefungua kesi hiyo dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Kibatala amesema, watanzania hao wanapinga  vifungu vya 7 (1) na (2) (c), (4) (a) na (6) vya Sheria ya Uraia ya Tanzania iliyofanyiwa marekebisho 2002 na kifungu cha 23 (1) (h) na (1) na cha 27 (2) (a) cha Sheria ya Uhamiaji iliyofanyiwa marekebisho 2016, wakidai vinakwenda kinyume na katiba ya nchi.

“Watanzania hao wanapinga vifungu vya sheria vinavyoelekeza kwamba raia yeyote wa Tanzania anayechukua uraia wa nchi nyingine, moja kwa moja anakuwa amepoteza uraia wa Tanzania.

Wamefungua kesi ya kikatiba kulalamika na kuiomba mahakama itamke kwamba vifungu kadhaa vya Sheria ya Uraia ambavyo kwa ufupi vinakataza uraia pacha, ni batili vinakiuka haki ya kikatiba ambayo hainyang’anyiki, haki ya kuwa raia wa kuzaliwa,” amedai Wakili Kibatala.

Wakili huyo amedai kuwa, katika kesi hiyo waleta maombi wataieleza mahakama hiyo namna wanavyoathirika na kukosekana kwa uraia pacha, ikiwemo kukosa haki ya kumiliki mali nchini Tanzania kwa mtu anayechukua uraia wa nchi nyingine.

“Tuweke wazi kwamba katiba yetu haitamki raia ni nani, lakini inatoa haki fulani kwa raia ikiwemo haki ya kushiriki kwenye mambo ya uongozi, kumiliki mali, kupiga kura, kwenda kokote utakako.

“Sisi mawakili wa waleta maombi tunaiomba mahakama itamke kwamba vifungu hivyo vinavyowanyang’anya haki ya kuwa raia wa Tanzania na haki nyingine za kikatiba, itamke kwamba ni batili,” amedai Wakili Kibatala.

3 Comments

  • Serikali ya Tanzania, baada ya miaka 61 ya uhuru, hatujui inaogopa nini kuhusu swala la uaraia pacha. Ila kitu kimoja mimi ninacho amini ni kua serikali ya Tanzania haijali kabisa kabisa watanzania wake waishio nje (au ughaibuni). Kuna waziri mmoja na profesa wwa sheria chuo kikuu (naye pia aliwahi kusomea Ujerumani) alisikika akiwahutubia watanzania waishio marekani kuwa utata wa uraia pacha unatokana na watanzania waishio Tanzania nao wanaomba uraia pacha wa nchi zao. Mimi sioni uhusiano wa watanzania waishio ughaibuni na hao waishio Tanzania. Watanzania waishio Tanzania niwajibu wao kuomba uraia pacha toka nchi zao na sio Tanzania.

    Wazawa wa Tanzania hawahitaji hadhi maalum, kwani kufanya hivyo ni sawa na kupoteza haki ya kuzalia katika nchi yako. Kigugumizi kikuba ninacho ona mimi ni kuwa serikali inaogopa sana kutoa uraia pacha, kwani ikifanya hivyo, wazanzibar-waomani wengi watarudi, na kama wakirudi wanaweza kuleta machafuko ya kisiasa na hasa ya muungano. Na hii ndiyo sababu halisi serikali ya Tanzania inaogopa kutoa uraia pacha

  • Kwenye uraia ndio unaweza kuelewa sisi wa tz tunashida gani? Kwa nini katiba ndio inaachwa kufuatwa? Vitabusho vya NIDA shida! uraia pacha je? eeh..!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

Habari Mchanganyiko

DC ampongeza Dk. Rose Rwakatare kwa kusaidia waathirika wa mafuriko Mlimba

Spread the loveMWENYEKITI wa Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk.  Rose Rwakatare...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the loveMBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi...

error: Content is protected !!