Saturday , 25 March 2023
Home Kitengo Michezo Diamond Platnumz ambwaga Mobeto mahakamani
Michezo

Diamond Platnumz ambwaga Mobeto mahakamani

Picha kubwa Hamisa Mobeto. Ndogo kulia mtoto wake Prince Abdul aliyezaa na Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz (kushoto)
Spread the love

MSANII Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ amemgalagaza mzazi mwenzake, Mwanamitindo Hamisa Mabeto katika kesi ya madai aliyoifungua katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kudai matunzo ya mtoto Prince Abdul, anaandika Angel Willium.

Hakimu Devotha Kisoka wa Mahakama hiyo ametupilia mbali madai ya Mobeto katika kesi hiyo baada ya kusikiliza hoja za pande hizo mbili husika.

Diamond aliwasilisha pingamizi dhidi ya kesi hiyo iliyofunguliwa na Mobeto akidai kuwa kesi hiyo imefunguliwa kwa kutumia kifungu ambacho si sahihi. Hoja ambayo ilipingwa na Mobeto.

Mobeto alifungua kesi hiyo mahakamani hapo, pamoja na mambo mengine anaiomba matunzo ya mtoto waliozaa na msanii Diamond.

Mwanamitindo huyo pia anaiomba mahakama imwamuru Diamond kutoa matunzo ya mtoto ya kila mwezi na alifungua kesi hiyo kupitia mawakili wake Abdullah Lyana na Walter Godluck kutoka kampuni ya uwakili ya Century Attorneys.

Kupitia hati hiyo ya madai, Mobeto anaomba Diamond amuombe msamaha kwa kumsababishia madhara yaliyoishtua familia yake.

Diamond aliwasilisha hati ya majibu hayo kinzani akipinga maombi hayo ya Mobeto akidai gharama anazodai kulipwa kwa mwezi ya Tsh. 5 milioni kwa ajili ya matunzo ya mtoto ni kubwa hawezi kuzimudu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Yanga: Fedha za Rais Samia zinaleta ari kubwa

Spread the loveUONGOZI wa klabu ya Yanga, umesema fedha zinazotolewa na Rais...

Michezo

Simba Sc. yamvulia kofia Rais Samia, yamuahidi makubwa dhidi ya Horoya

Spread the loveWAKATI timu ya Simba ikiibuka na ushindi wa bao 3-0...

Michezo

Taasisi ya TKO na TFF yawapiga msasa makocha wa kike 54

Spread the love WAKATI Soka la wasichana likichipua kwa kasi Taasisi ya...

Michezo

Kimwanga CUP yazidi kutimua vumbi

Spread the loveMASHINDANO ya mpira wa miguu ya Kimwanga CUP ya kuwania...

error: Content is protected !!