December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Diamond Platnumz amfanyia kufuru Aristotle

Spread the love

 

NI kufuru! Ndicho alichokifanya Staa wa Bongofleva, Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnumz katika harusi ya mpambaji maarufu wa wasanii wa kike, Aris Mwamtobe ‘Aristote’ baada kutumia zaidi ya Sh milioni 180 katika harusi hiyo iliyokuwa gumzo nchini. Anaripoti Matilda Buguye, Dar es Salaam … (endelea).

Harusi hiyo ya kifahari iliyohudhuriwa na mastaa wa tasnia zote nchini ilifanyika usiku wa kuamkia leo tarehe 21 Novemba, 2021 katika ukumbi wa Sea Breez – Mbezi beach jijini Dar es salaam.

Katika harusi hiyo iliyosimamiwa na Mfanyabiashara Fred Ngajiro maarufu Fred Vunjabei aliyekuwa Mwenyekiti wa kamati,  ilishuhudiwa mastaa wakivunja kabati kwa kuonesha viwalo vya aina yake.

Aidha, kwa upande wake Diamond platnumz aliyehudhuria sherehe hiyo mlimfanyia kufuru bwana harusi – Aristote’ ambaye anajiita ‘chawa  wa Mondi’ kwa kumwagia zawadi za aina yake na kuwaacha midomo wazi wageni waalikwa katika sherehe hiyo ya kukata na shoka.

Msanii Diamond alimkabidhi Aristote pesa taslimu Sh milioni 15, hundi ya thamani ya Shmilioni 15, pamoja na kiwanja kilichopo Kigamboni pembezoni mwa bahari chenye thamani ya Sh milioni 50.

Diamond hakuishia hapo, bali alirusha mubarasha sherehe hiyo kupitia runinga yake ya Wasafi Tv kwa muda usiopungua saa tano.

Baada ya kumalizika kwa sherehe hiyo, leo Diamond ameweka mchanganuo wa gharama alizotumia kwa Aristote kwamba mbali na fedha taslimu milioni 15, hundi ya Sh milioni 15, kiwanja cha thamani ya Sh milioni 15, pia gharama za kurusha harusi hiyo ni Sh milioni 100.

Msanii huyo ameweka wazi kuwa jumla ametumia Sh milioni 180.

error: Content is protected !!