December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Diamond kuwania tuzo za MTV EMA

Naseeb Abdul 'Diamond Platnum’

Spread the love

 

KIOO wa Bongofleva, Naseeb Abdul maarufu kama Diamond platnumz amechaguliwa kuwania tuzo za MTV EMA, akiwa ni msanii pekee kutokea Afrika mashariki kuwania tuzo hizo. Anaripoti Matilda Buguye, Dar es Salaam … (endelea)

Tuzo hizo zinazofahamika kama Europe Music Award (EMA) zinatarajiwa kutolewa tarehe 14, Novemba, 2021 huko nchini Hungary Barani Ulaya.

Aidha, moja kati ya vigezo vitakavyompa msanii nafasi ya kushinda ni kupigiwa kura kwa wingi kwa sababu unaruhusiwa kupiga kura mara nyingi uwezavyo na kumfanya msanii wako ashinde tofauti na tuzo za BET ambazo hawaruhusu upigaji kura.

Diamond anawania katika kipengele cha Msanii Bora Kimataifa (Best International Act) ambapo anapambana na wasanii wanne kutokea barani Afrika kama vile Wizkid (Nigeria), Tems (Nigeria) Focalistic (Africa Kusini) na Amaarae (Ghana).

Imekuwa ni desturi sasa kwa nyota huyu kuingia kwenye vinyang’anyiro vya tuzo karibu vyote aidha, kwa kushinda ama kutoshinda hakika anaiwakilisha vyema Tanzania na hata Afrika kiujumla.

Itakumbukwa tuzo hizi zilitoka kwa mara ya kwanza tarehe 24 November, 1994 huko Ujerumani.

error: Content is protected !!