October 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dhamana ya mwandishi Kabendera Agosti 5

Erick Kabendera

Spread the love

MAOMBI ya dhamana Namba 14 ya mwaka 2019 ya mwanahabari Erick Kabendera, yanatarajiwa kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam tarehe 5 Agosti 2019. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Uamuzi huo umetolewa leo tarehe 1 Agosti 2019 na Augustine Rwizile, Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya mawakili upande wa Jamhuri kuomba muda wa kuyapitia maombi hayo na kuwasilisha hati kinzani.

Maombi hayo ya dhamana yaliwasilishwa na mawakili wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), tarehe 31 Julai 2019 ikiwa ni siku mbili tangu Kabendera kukabidhiwa kwa Idara ya Uhamiaji akituhumiwa kuwa sio raia wa Tanzania.

Hadi sasa Kabendera anashikiliwa na Uhamiaji kwa ajili ya mahojiano kuhusu.

Katika maombi hayo, mawakili wa Kabendera, Catherine Ringo na Shilinde Swedy wameiomba mahakama iamuru mteja wao afikishwe mahakamani au apewe dhamana na polisi.

error: Content is protected !!