SAA chache kabla ya Simba ya Dar es Salaam, kushuka dimbani kuumana na Dodoma Jiji, aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa timu hiyo, Mohamed Dewji amewapa ujumbe wachezaji. Anaripoti Damas Ndembela, TUDARCo … (endelea).
Leo Ijumaa saa 10:00 jioni, katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, inashuka dimbani katikamchezo wa pili wa ligi hiyo.
Mchezo wa kwanza, Simba ilitoka sare ya kutofungana na Biashara United, Uwanja wa Karume,Musoma mkoani Mara huku Dodoma Jiji yenyewe ikiiibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting, katika uwanja wake wa nyumbani.
Wachezaji wa Simba wanapaswa kukumbuka kuwa wanashikilia maisha na furaha ya watu. pic.twitter.com/snRt640nGT
— Mohammed Dewji MO (@moodewji) October 1, 2021
Simba itakuwa inashuka dimbani kutafuta ushindi wa kwanza katika michezo mitatu iliyocheza pasina kushika ikitanguliwa na ule wa TP Mazembe uliomalizika kwa kipigo cha 1-0 siku ya kilele cha Simba Day na kipigo kingine cha 1-0 kutoka Yanga kwenye mechi ya Ngao ya Jamii.
Kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Twitter, Dewji ambaye ni mwekezaji ndani ya timu hiyo ameweka picha akizungumza na wachezaji wa Simba na kuandika ” wachezaji wa Simba wanapaswa kukumbuka kuwa wanashikilia maisha na furaha ya watu.”
Leave a comment