November 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dewji afikia kikomo cha uvumilivu Simba

Mohammed Dewji 'MO'

Spread the love

MOHAMMED Dewji ‘Mo’ Mwekezaji wa klabu ya Simba, ameweka wazi kuwa klabu hiyo haitamvumilia mchezaji yeyote atakayeihujumu timu hiyo. Anaripoti Faki Sosi …(endelea).

Hayo ameyeweka wazi leo tarehe 8 Desemba 2019, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter, amesema kuwa uongozi wa klabu hiyo unawalipa wachezaji hao hivyo nao wanatakiwa kuwajibika.

“Sisi tunawalipa vizuri mno, na wao wana wajibu wa kutulipa matokeo na furaha. Na ili furaha iwepo, lazima nidhamu isimamiwe kikamilifu, na katika hili hatutanii. Hatutajali ukubwa wa jina la mchezaji yoyote.” amesema ‘Mo’

Amesema kuwa matokeo mabaya kwa klabu hiyo itakuwa ndio mwisho wa uvumilivu wake.

“Simba lazima tuamue kuteseka na moja katika mambo haya mawili: (1) tuzoee uchungu na maumivu ya nidhamu au (2) maumivu ya matokeo mabaya. Kama mpenzi wa Simba, siwezi kujitoa wala kuvumilia matokeo mabaya kwa sababu ya mapungufu ya nidhamu.”

error: Content is protected !!