Friday , 29 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Gari lililomteka MO hili hapa
Habari MchanganyikoTangulizi

Gari lililomteka MO hili hapa

Spread the love

MKUU wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro amesema polisi wamefanikiwa kumtambua dereva na  gari lililohusika katika tukio la kutekwa mfanyabiashara Mohammed Dewji maarufu kama ‘Mo Dewji.’ Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

IGP Sirro ameyasema hayo leo tarehe 19 Oktoba 2018 wakati akizungumza na wanahabari kuhusu tukio hilo lililotokea tarehe 11 Oktoba mwaka huu, katika hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam.

Kamanda Sirro ameeleza kuwa, uchunguzi uliofanywa na Jeshi la Polisi umebaini kuwa, gari lililotumika kumteka Mo Dewji limetokea nchi jirani.

“CCTV Camera zimetusaidia tumeweza kutambua gari mara ya kwanza sababu ilikuwa asubuhi hatukuweza kutambua vizuri baada ya vyombo vyetu kufanya uchunguzi tumeweza kutambua kwamba linawezekana ndilo gari lililohusika katika hili tukio,” amesema na kuongeza Kamanda Sirro

“Gari hili limetokea nchi jirani na watu wetu wamekwenda mpaka mpakani na gari hii ilipita kwenye mpaka huo tarehe 1 September 2018, tumepata details za kutosha, nani mwenye gari nchi anayotoka imefahamika, watu wetu wa Interpol wanafanyia kazi.”

Licha ya uchunguzi kubaini kwamba gari na mmiliki wake anatokea nje ya nchi, Kamanda Sirro amesema kwa sasa Jeshi la Polisi haliwezi kutaja nchi ambayo gari hilo limetoka.

“Suala yuko hai au hayuko hai sina jibu, ningekuwa mimi nimteka ningejua yuko hai au hayuko hai, mpaka tukipata watuhumiwa tutajua lengo lao nini, nchi ni mapema kuitaja, nikiitaja tutafuta uhasama na nchi fulani, suala la gari kurudi au kutoka sina majibu, mtu akipata taarifa kuhusu hiyo gari atusadie,” amesema.

Katika hatua nyingine, Kamanda Sirro amesema Jeshi la Polisi limezifanyia uchunguzi risasi mbili zilizookotwa katika eneo lililotokea tukio, kwenye maabara ya polisi.

“Huyu anaetaka kuiharibu nchi yetu tukimkata atajua hii ni Tanzania, mpaka sasa tumebaki na watu wanane, kati ya 27 waliokuwa wamekamatwa ambao tuna sababu ya kuendelea kupeleleza, tunapokea mawazo ya kujenga, yasiyokuwa ya kujenga hayatusaidii, kama unamawazo mazuri ya kumsaidia Mo tunayapokea,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanafunzi Nyamkumbu wanolewa na GGML kuhusu taaluma ya madini

Spread the loveZAIDI ya Wanafunzi 50 kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana...

Habari Mchanganyiko

Somo la dini: Waislamu waishukia Serikali, wizara yatoa kauli

Spread the loveJUMUIYA na Taasisi za Kiislamu Tanzania, imetupia lawama Serikali ikidai...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

error: Content is protected !!