Spread the love

 

HATIMAYE mabingwa wa kihistoria wa soka nchini Tanzania, Yanga ya jijini Dar es Salaam, imemtambulisha Danis Nkane. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Nkane anayecheza nafasi ya kiungo mahambuliaji, ametambulishwa leo usiku Jumamosi, tarehe 1 Januari 2022, kupitia kuraza za kijamii za Yanga.

Nkame amejiunga na miamba hao wa soka la Tanzania akitokea Biashara United ya mkoani Mara, alikoonesha uwezo mkubwa wa kusakata kandanda.

Ni kijana wa Kitanzania mwenye kipaji cha pekee anayeweza kukimbia na mpira kwa ufundi wa hali ya juu.

Mchezaji wa zamani wa Yanga, Mrisho Ngassa amenukuliwa akimzungumzia kuwa staa wa baadaye huku akiuomba uongozi wa timu hiyo kumpa jezi namba 16 aliyokuwa akiivaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *