March 5, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Deni la taifa lazidi kupaa

George Simbachawene

Spread the love

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti imewasilisha taarifa ya mwaka kuhusu utekelezaji wa majukumu yake katika kipindi cha Januari, 2018 hadi Januari 2019 huku ikionesha kuongezeka kwa deni la taifa. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Aidha kamati hiyo imebaini kukua kwa deni la taifa likijumuisha fedha zilizokopwa na serikali kutoka katika vyanzo vya ndani na nje pia na sekta binafsi kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo.

Akiwasilisha taarifa ya Kamati ya Bunge leo 2 Februari 2019 bungeni jijini Dodoma, mwenyekiti wa kamati hiyo, George Simbachawene amesema, hadi kufikia Novemba 2018 deni la taifa limeendelea kukua taratibu hadi kufikia Sh 61.8 trilioni.

Pamoja na hayo amesema, ukuaji wa deni hilo umetokana na mahitaji ya uwekezaji kwenye miradi ya maendeleo na kijamii nchini kwa ajili ya kukuza uchumi.

“Kamati inashauri serikali kuangalia uwiano uliopo kati ya mwenendo wa upatikanaji wa mapato ya ndani pamoja na ulipaji wa deni la serikali na athari zake katika bajeti na uchumi,” amesema.

error: Content is protected !!