January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Deni la MSD laitesa serikali

Maboski ya dawa kutoka Bohari ya Madawa Tanzania (MCD)

Spread the love

SERIKALI imesema hospitali nyingi za Umma hapa nchini zinapata huduma ya dawa, vifaa tiba,vifaa na vitenganishi kupitia Bohari Kuu ya Dawa (MSD). Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Hata hivyo imeelezwa vituo vingi vya umma vimekuwa vikidaiwa  deni kubwa na bohari hiyo  kutokana na ufinyu wa bajeti ambapo kiasi cha fedha kinachotengwa hakilingani na mahitaji halisi ya vituo vya kutolea huduma husika.

Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Seif Rashidi alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Viti Maalum, Riziki Omar Juma(CUF).

Mbunge huyo alitaka kujua ni lini serikali italipa deni la MSD ili vifaa viweze kupatikana bila masharti.

“Taasisi ya mifupa MOI ina deni la sh.bilioni moja kwa MSD mpaka sasa imefikia kufungiwa kupata vifaa bila kutoa fedha.

“Je ni lini serikali italipa deni hilo ili vifaa viweze kupatikana bila masharti” alihoji Juma.

Akijibu swali hilo Dk.Seif,amesema  hadi kufikia Juni 30 mwaka huu deni la MOI kwa MSD limefikia bilioni 1.1 katika kukubaliana na changamoto za ukuaji wa deni hilo na upatikanaji wa dawa katika taasisi hiyo.

Amesema  serikali inaendelea kupunguza deni hilo kulingana na upatikanaji wa fedha ambapo katika kipindi cha Aprili hadi Juni kiasi cha sh. Milioni 71 zimepelekwa MSD ili kuiwezesha taasisi ya MOI kupata mahitaji.

error: Content is protected !!