January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Defao afariki dunia

Spread the love

 

Nguli wa muziki wa Rhumba kutoka Congo, Général Defao (63) amefariki dunia nchini Cameroon alikokwenda kutumbuiza. Anaripoti Mwandishi Wetu  … (endelea).

Defao ambaye jina lake ni Lulendo Matumona amefariki jana tarehe 27 Disemba, 2021 katika hospitali ya Laquintinie iliyopo mjini Douala nchini Cameroon.

Mkongwe huyo ambaye alitarajiwa kutumbuiza katika mkesha wa mwaka mpya, inadaiwa alipotua nchini humo alianza kuugua ghafla ambapo vyanzo vya ndani vinaeleza alikua na matatizo ya kisukari na maambukizi ya Corona.

Mwanamuziki huyo aliyetarajiwa kusherehekea ‘birthday’ yake Tarehe 31 Disemba mwaka huu, alitambulika rasmi kwenye muziki mwaka 1976.

Alifyatua nyimbo kali kama vile Sidewalk radio, Kikuta family na School love.

error: Content is protected !!