August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

DED amwaga chozi mbele ya LAAC

Spread the love

AGNESS Mkandya, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Gairo (DED), Morogoro amemwaga machozi mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) baada ya kubanwa maswali na wanakamati hiyo, anaandika Dany Tibason.

Wakati akimwaga machozi, Mkandya alikuwa akilalamika kwamba, halmashauri hiyo ina watumishi wasio waaminifu.

Kati ya maswali ambayo yalimfanya Mkandya kumwaga machozi ni pamoja na lile la Reah Komanya, Mbunge wa Viti Maalum (CCM) aliyemtaka kueleza sababu za halmashauri hiyo kushindwa kujipanga katika kusimamia mapato.

“Halmashauri ya Gairo ina mpango gani mkakati wa kuunganisha mfumo wa udhitibiti wa ndani.
“Eneo la ubadhirifu si ukusanyaji wa mapato pekee bali pia matumizi ya mfumo mzima wa “EPICOR.”

“Ubadhirifu unaweza kuwemo kutokana na kutokusanya mapato kwa mfumo wa kielektroniki na kutokuwepo kwa ‘data bese’.

“Utunzaji wa mali za halmashauri mfano wa kuweka alama madawati yanayochangwa na wadau mbalimbali na mfumo mzima wa uidhinishaji wa matumizi ya umma,” amehoji Komanya.

Mkurugenzi huyo alishindwa kujibu maswali hayo huku akiangua kilio jambo lililoifanya kamati kudai kuwa, suala hilo litatolewa maagizo na kamati.

Hata hivyo, mkurugenzi huyo amesema licha ya kuwa ni mgeni katika halmashauri hiyo, alikuta halmashauri ikiwa na uchafu mkubwa kutokana na kuwepo kwa watumishi wabadhirifu wa mali ya umma.

Amesema, mpaka sasa watumishi wa idara mbalimbali katika Halmashauri ya Gairo wapatao tisa wamesimamishwa kazi kutokana na ubadhirifu huku uchunguzi ukiendelea.

Hata hivyo Rosse Kamili Mjumbe wa Kamati hiyo ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) amehoji sababau za halmashauri hiyo imeshindwa kutumia asilimia tano kwa ajili ya akima mama pia asilimia tano kutofika kwa vijana.

error: Content is protected !!