August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Deby ashinda tena urais Chad

Spread the love

TUME ya Uchaguzi nchini Chad (CEN) leo imemtangaza Idriss Deby kuwa mshindi wa kiti cha urais, anaandika Pendo Omary.

Deby ambaye pia ni Mwenyekiti wa mpya wa Umoja wa Afrika (AU) ameshinda uchaguzi huo kwa kupata asilimia 61.56 ya kura huku mpinzani wake wa karibu Saleh Kebzabo akifuatia kwa kupata asilimia 12.80 ya kura.

Nafasi ya tatu imeshikwa na Laokein Kourayo Mbaiherem kwa kupata asilimia 10.60 ya kura.

Duru ya kwanza ya Uchaguzi Mkuu ilifanyika tarehe 10 Aprili mwaka huu ambapo matokeo yasiyokuwa rasmi yalidhihirisha ushindi wa Deby dhidi ya wagombea wengine 12.

Deby ndiye mwanzilishi wa chama tawala cha Patriotic Salvation Movement kilichoanzishwa mwaka 1990 na meongoza nchi hiyo kwa miaka 26 tangu aliponyakua madaraka katika mapinduzi.

Baadaye Rais Deby alichaguliwa tena kwenye uchaguzi wa mwaka 1996, 2001, 2006 na 2011. Hata hivyo upinzani nchini Chad umetilia shaka ushindi huo.

Serikali nchini humo imepiga marufuku maandamano ya kumtaka Deby aondoke madarakani ambapo baadhi ya wanaharakati tayari wamefungwa.

error: Content is protected !!