Thursday , 2 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko DCEA yakamata kilo 16.643 za dawa za kulevya, washirika wa Cambiaso ndani
Habari Mchanganyiko

DCEA yakamata kilo 16.643 za dawa za kulevya, washirika wa Cambiaso ndani

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Gerald Kusaya
Spread the love

 

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imekamata jumla ya kilo 16.643 za dawa ya kulevya zikijumuisha kilo 15.19 za heroin, gramu 655.73 za cocaine na gramu 968.67 za Methamphetamine zilizowahusisha jumla ya watuhumiwa saba. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Ukamataji wa kilo 15.19 za dawa za kulevya aina ya heroin zilizowahusisha watuhumiwa watatu ni mwendelezo wa operesheni zilizopita.

Watuhumiwa hao ni washirika wa Kambi Zuberi Seif ‘Cambiaso’ na wenzake waliokamatwa wakiwa na kilo 34.89 za heroin katika operesheni ya mwanzoni mwa mwezi Novemba 2022.

Katika taarifa iliyotolewa leo tarehe 7 Disemba, 2022 na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – DCEA, Florence Khambi amewataja watuhumiwa hao watatu kuwa ni Suleiman Thabit Ngulangwa (36), mfanyabiashara na mkazi wa Salasala.

Sharifa Seleman Bakar (41), mkazi wa Maji matitu – Mbagala na Farid Khamis Said (22) mkazi wa Maji matitu – Mbagala, wote ni wakazi wa Dar es Salaam.

Amesema watuhumiwa wengine wanne walikamatwa wakiwa na gramu 655.75 za cocaine na gramu 968.67 za Methamphetamine.

Amesema watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa kwenye harakati za kusafirisha dawa hizo za kulevya kwenda nje ya nchi.

“Watuhumiwa hao wanne ni Hussein Rajab Mtitu (28) anayejulikana pia kama Chodri Mohamed mfanyabiashara na mkazi wa Kibonde maji, Mbagala, Jaalina Rajab Chuma (31) anayejulikana pia kama Jaalina Mohan mjasiriamali na mkazi wa Tandika.

“Shabani Abdallah Said (36) mkazi wa Kilimahewa, Tandika, hawa pia ni wakazi wa Dar es Salaam, pamoja na Irene Dickson Mseluka (39) mfanyabiashara na mkazi wa Ndala Shinyanga,” amesema.

Amesema watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa na watafikishwa mahakamani mara baada ya taratibu za kiupelelezi kukamilika.

Aidha amesema kutokana na kuimarika kwa udhibiti wa dawa za kulevya nchini, wahalifu wa dawa za kulevya wamekuwa wakibuni mbinu mbalimbali ili kufanikisha uhalifu wao.

Hata hivyo, amesema mamlaka iko macho na inaendelea kukabiliana na mabadiliko ya mbinu hizo.

“tunashirikiana na makampuni ya usafirishaji wa vifurushi, vyombo vyote vya ulinzi na usalama na wadau wengine katika udhibiti na mapambano dhidi ya dawa za kulevya ili kukabiliana na mbinu mpya za usafirishaji na uuzaji wa dawa za kulevya,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

GGML kuwapatia mafunzo kazi wahitimu 50 wa vyuo vikuu nchini

Spread the loveJUMLA ya wahitimu 50 wa vyuo vikuu nchini wamepata fursa...

Habari Mchanganyiko

NHC yaongeza mapato kufikia kufikia Sh bilioni 257

Spread the loveSHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limeongeza mapato hadi kufikia...

Habari MchanganyikoTangulizi

Mo Dewji achomoza bilionea pekee Afrika Mashariki

Spread the loveMAZINGIRA mazuri ya uwekezaji nchini Tanzania yamezidi kuleta matunda baada...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia: Panapotokea uvunjifu wa amani panakuwa haki imepotezwa

Spread the love  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu...

error: Content is protected !!